Skip to main content

WADAU SINGIDA WAJADILI UPATIKANAJI ELIMU, MAARIFA YA MSINGI KWA WANANCHI

Na Saulo Stephen - Singida.

WADAU SINGIDA WAJADILI UPATIKANAJI ELIMU, MAARIFA YA MSINGI KWA WANANCHI

Na Saulo Stephen - Singida.

Katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima kwa mwaka 2026 kwa ngazi ya Mkoa, wadau wa elimu Manispaa ya Singida wamekutana kujadili namna ya kuimarisha upatikanaji wa elimu na maarifa ya msingi kwa wananchi.

Katika maandalizi hayo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Tumaini - Viziwi, Manispaa ya Singida, washiriki walijadiliana mafanikio yaliyopatikana, changamoto zilizopo na mikakati ya kuendeleza mpango wa K.K.K (Kusoma, Kuandika na Kuhesabu), kwa lengo la kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma.

Majadiliano hayo yamelenga pia kuimarisha ushiriki wa wadau mbalimbali katika utoaji wa elimu ya watu wazima, sambamba na kutathmini namna elimu hiyo inavyoweza kuchangia kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo na kuboresha ustawi wa jamii.

Kilele cha Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima kwa ngazi ya Mkoa wa Singida kinatarajiwa kufanyika Septemba 16, 2026 katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi, chini ya kauli mbiu isemayo, “Kusoma kwa Maarifa ya Watu Duniani na Ustawi wa Jamii.”

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.