Skip to main content

WACHIMBAJI WADOGO KANDA YA ZIWA WAJENGEWA UWEZO KINGA YA MAJANGA UJIO MVUA ZA EL-NINO

Wizara ya madini kupitia tume ya madini leo tarehe 28 september 2026 imeendesha mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika mikoa ya kimadini katika ukanda wa ziwa victoroa kwa ajili ya maandalizi ya kukabiliana na athari za mvua za elnino zinazotarajiwa kunyesha juu ya wastani mwanzoni mwa mwezi October 2026.

WACHIMBAJI WADOGO KANDA YA ZIWA WAJENGEWA UWEZO KINGA YA MAJANGA UJIO MVUA ZA EL-NINO
Studio Narration JAMBO FM

WACHIMBAJI WADOGO KANDA YA ZIWA WAJENGEWA UWEZO KINGA YA MAJ...

0:00 --:--

Wizara ya madini kupitia tume ya madini leo tarehe 28 september 2026 imeendesha mafunzo kwa wachimbaji wadogo katika mikoa ya kimadini katika ukanda wa ziwa victoroa kwa ajili ya maandalizi ya kukabiliana na athari za mvua za elnino zinazotarajiwa kunyesha juu ya wastani mwanzoni mwa mwezi October 2026.

MHANDISI YAHAYA SAMABA KATIBU MKUU WIZARA YA MADINI

Mafunzo hayo ambayo yamefanyika katika ukumbi wa Malex uliopo katika manispaa ya Kahama mkoa wa Shinyanga yamewakutanisha wachimbaji wadogo kutoka katika maeneo ambayo mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) imeyataja kuathiriwa Zaidi ambayo ni mkoa wa kimadini Kahama Simiyu ,Mara Mwanza Tabora na Shinyanga.

Akifungua mafunzo hayo katibu mkuu wizara ya madini Mhandisi Yahaya Samamba amesema serikali imetathimini na kuona si vyema kupuuza janga hilo la elnino linalotarajiwa kutokea na ndiyo maana imeona vyema kuwakutanisha wachimbaji katika mikoa yote inayotarajiwa kuwa na athari zaidi ili kujadiliana kwa pamoja namna ya kukabiliana na janga hilo.

Samamba amesema asimia 70 ya ajali katika migodi mingi ya dhahabu hutokana na udongo kuwa mzito na kuanguka ambako husababishwa na wachimbaji kuchumba pasipo kufata matimba,pamoja na matumizi holela ya baruti na mafuriko ya maji katika maduara ya dhahabu hivyo elimu hiyo itakwenda kunusuru vifo vya wachimbaji kwa asilimia 70 katika msimu wa mvua

Aidha Samamba amewatka viongozi katika migodi husika kuunda sheria ndogogo zitakazochochea uwajibikaji wa lazima katika kujikinga na majanga ikiwamo kuzuia wachimbaji kustisha shughuli zao wakati mvua ikinyesha pamoja na kuwa na masaa machache ya uchimbaji ili kutopunguza umakini kwa wachimaji hao na kutoa taarifa za mapema mara wanapoona viashira vya hatari

Amewataka pia maafisa madini kusimamia maelekezo yote yanatolewa na serikali pamoja na sheria zilizotungwa na mgodi husika ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wachimbaji kwa upendo katika kukabiliana na majanga huku akiongeza kuwa mgodi wowote utakaoshindwa kutekeleza majukumu ya uchukuaji tahadhari serikali haitasita kuufunga.

GREGORY KIBUSI NAIBU KATIBU MKUU SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WACHIMBAJI TANZANIA

Kwa upande wake naibu katibu mkuu wa shirikisho la vya wachimbaji nchini (FEMATA) Gregory Kibusi ameiomba serikali kupitia fedha zilizotengwa kwa ajili ya athari za enino kununua ununuzi wa vifaa vya kisasa vya uokoaji ikiwemo pump kubwa ya kuvuta maji ili kukabiliana na majanga endapo yatatokea, huku akiwataka wachimbaji wadogo kujenga kingo za kuzuia maji na kutengeneza mifereji ya kuchepusha maji ili yasiiingie ndani ya migodi ili kuepuka athari zitikanazo na mvua hizo.

Nao baadhi ya wachimabji wadogo walioudhuria mafunzo hayo akiwemo Juma Sarungi ameishukuru kwa elimu hiyo na kwamba tayari walikuwa wameshaanza kuchukua hatua kwa kuchimba mitaro katika maeneo ya migodi yao sambamba na kununua pampu kubwa za kuvuta maji hivyo kuongezwa elimu hiyo imekuwa na tija kwao

JUMA SARUNGI MMILIKI WA MGODI

Naye Eva Jerad ameipogeza wizara ya madini kwa elimu hiyo na kwamba itakwenda kuwasaidia kupambana na majanga ili mvua hizo zisiende kuleta madhara makubwa ikiwemo vifo

EVA JERAD MCHIMBAJI MDOGO

WACHIMAJI WADOGO WAKIFUATILIA MAFUNZO JUU YA KUKABILIANA NA MAJANGA YATOKANYO NA MVUA ZA ELNINO

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.