Skip to main content

WACHIMBAJI WA MADINI SINGIDA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

Wachimbaji wa madini na wadau wa sekta hiyo mkoani Singida wametakiwa kuzingatia sheria za uchimbaji, kuepuka migogoro na kutumia fursa zilizopo kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.

WACHIMBAJI WA MADINI SINGIDA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA
Studio Narration JAMBO FM

WACHIMBAJI WA MADINI SINGIDA WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA

0:00 --:--

Wachimbaji wa madini na wadau wa sekta hiyo mkoani Singida wametakiwa kuzingatia sheria za uchimbaji, kuepuka migogoro na kutumia fursa zilizopo kukuza uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, wakati akizungumza katika kikao kilichofanyika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, ambapo amesisitiza umuhimu wa kufanya shughuli za uchimbaji kwa amani, uadilifu na kufuata taratibu zilizowekwa na Serikali.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego akizungumza katika kikao cha Wachimbaji na wadau wa Madini Mkoani humo.

Aidha, amewahimiza wachimbaji kutumia msaada wa kisheria kabla ya kusaini mikataba, kuuza madini kupitia mifumo inayotambulika na kuwekeza mapato yao katika shughuli nyingine za kiuchumi.

Wachimbaji na Wadau wa Madini Mkoani Singida walipohudhuria kikao na Mkuu wa huo Halima Dendego.

Kwa upande wake, Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Singida, Mhandisi Sabai Nyansiri, na wakilishi wa wachimbaji wameelezea umuhimu wa ushirikiano, matumizi ya teknolojia na utatuzi wa changamoto za umeme, barabara na tozo ili kuimarisha sekta ya madini.Wachimbaji na Wadau wa Madini Mkoani Singida walipohudhuria kikao na Mkuu wa huo Halima Dendego.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.