Skip to main content

WAASWA KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI BADALA YA KUTEGEMEA MISAADA

Na Clavery Christian, Biharamulo - Kagera.

WAASWA KUTUMIA FURSA ZA KIUCHUMI BADALA YA KUTEGEMEA MISAADA

Na Clavery Christian, Biharamulo - Kagera.

Viongozi wa Halmashauri wa Wilaya ya Biharamulo wamehimizwa kuacha tabia ya kutegemea kuomba fedha pekee kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo, badala yake waelekeze nguvu zao katika kutafuta na kutumia fursa zilizopo ndani ya maeneo yao ili kuleta maendeleo endelevu.

Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Kagera ndugu Faris Buruhani wakati wa majadiliano kuhusu utekelezaji wa shughuli za maendeleo, ambapo viongozi walikumbushwa umuhimu wa ubunifu na ushirikishwaji wa wadau katika kuibua na kutumia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika sekta mbalimbali.

Ndugu Farisi alieleza kuwa ushiriki wa vijana katika shughuli za uzalishaji mali, biashara na miradi ya maendeleo ni muhimu katika kujenga uchumi imara na kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla.

Aidha, Kamati ya Utekelezaji imeendelea kuhamasisha vijana pamoja na wadau wa maendeleo kuchangamkia fursa hizo kwa vitendo, ikieleza kuwa matumizi sahihi ya fursa zilizopo yanaweza kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya wananchi.

Wadau nao wamehimizwa kushirikiana na serikali katika kubaini na kuendeleza fursa mbalimbali za kiuchumi ili kuhakikisha maendeleo yanayopatikana yanakuwa na manufaa ya muda mrefu kwa wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.