Skip to main content

WAANDISHI KAGERA WAPATIWA MAFUNZO UWASILISHAJI HABARI KIDIJITALI

Na Cecilia Shiratu, Bukoba - Kagera.

WAANDISHI KAGERA WAPATIWA MAFUNZO UWASILISHAJI HABARI KIDIJITALI

Na Cecilia Shiratu, Bukoba - Kagera.

Waandishi wa Habari Mkoani Kagera, wamepatiwa mafunzo kuhusu uwasilishaji wa habari kijigitali na za mtandaoni, kwa lengo la kuwawezesha kuwasilisha taarifa sahihi na zinazozingatia kanuni na maadili ya uandishi.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na kutolewa na Kampuni ya Media Brains kwa kushirikiana na taasisi ya Konrad Adenauer Stiftung (KAS), yanalenga kuwajengea uwezo Waandishi katika kukabiliana na mabadiliko yanayoendelea katika sekta ya habari, hususan matumizi ya majukwaa ya kidigitali.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkuu wa Usimamizi wa Ugavi na Usafirishaji wa Media Brains, Neville Meena alisema, Waandishi wana wajibu wa kuhakikisha taarifa wanazozitoa kwa umma zina ukweli na uhakika.

Amesema, mafanikio ya Mwandishi katika ulimwengu wa kidigitali yanategemea uwezo wake wa kuwasilisha maudhui yenye usahihi, kwa kuepuka makosa yanayoweza kupotosha umma, hasa katika kipindi ambacho habari husambaa kwa kasi kupitia mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali ya mtandaoni.

Kwa upande wake, Afisa Mkuu wa Uendeshaji wa Media Brains, Absalom Kibanda ametoa elimu kuhusu namna bora ya kuwasilisha taarifa kwa umma, kupitia mitandao ya kijamii.

Amesisitiza umuhimu wa Waandishi kuelewa matumizi sahihi ya majukwaa ya kidigitali, ili kuyatumia kama nyenzo ya kufikisha taarifa kwa jamii kwa haraka, bila kuathiri misingi ya taaluma ya uandishi wa habari.

Mafunzo hayo, yanatarajiwa kuwasaidia Waandishi wa habari mkoani Kagera kuongeza ujuzi na uwezo wa kuandaa na kusambaza maudhui ya kidigitali, kwa kuzingatia maadili na kanuni za taaluma, kwa lengo la kuhakikisha Wananchi wanapata taarifa sahihi na za kuaminika.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.