Skip to main content

WAAMUZI WAIMALIZA SINGIDA JOURNALIST FC MECHI YA KIRAFIKI, NI KICHAPO CHA 4-1

Timu ya soka ya waandishi wa habari Mkoa wa Singida, Singida Journalist FC, imekubali kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya timu ya waamuzi Mkoa wa Singida katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Jumapili, Oktoba 11, 2026, katika Dimba la chuo cha Ufundi VETA Singida, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Michuano ya Yagi Kiaratu Jimbo Cup.

WAAMUZI WAIMALIZA SINGIDA JOURNALIST FC  MECHI YA KIRAFIKI, NI KICHAPO CHA 4-1
Studio Narration JAMBO FM

WAAMUZI WAIMALIZA SINGIDA JOURNALIST FC MECHI YA KIRAFIKI,...

0:00 --:--

Timu ya soka ya waandishi wa habari Mkoa wa Singida, Singida Journalist FC, imekubali kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya timu ya waamuzi Mkoa wa Singida katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Jumapili, Oktoba 11, 2026, katika Dimba la chuo cha Ufundi VETA Singida, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Michuano ya Yagi Kiaratu Jimbo Cup.

Michuano hiyo inadhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Yagi Kiaratu. Licha ya matokeo hayo, Singida Journalist FC imeonyesha kiwango kizuri cha mchezo, ikiwategemea nyota wake Abdul Bandola, Robert Onesmo maarufu Robertinho, Amini Nyaungo ‘Kiraka’, Jamaldin Abuu, Johnson Soa, Elikana Obed na mlinda mlango Cales Katemana.

Nyota wa timu ya Singida Journalist FC Amini Nyaungo "Kiraka "akimiliki mpira kwenye himalayas yake

Katika mchezo huo, kiungo mshambuliaji Saulo Stephen, maarufu Sports Doctor, aliingia kipindi cha pili na kuongeza uhai katika safu ya ushambuliaji ya Singida Journalist FC, huku kikosi hicho kikiongozwa na kocha Ismail Abdallah. Timu hiyo sasa inaendelea na maandalizi yake kuelekea Michuano ya Yagi Kiaratu Jimbo Cup.Kiungo mshambuliaji wa Singida Journalist FC Saulo Stephen "Sports doctor.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.