Skip to main content

VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VIWE MACHO DHIDI YA WAVUNJA AMANI - DKT. MWIGULU

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kuwa macho dhidi ya vitendo vinavyolenga kuvuruga amani ya nchi huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kusimamia usalama wa wananchi na mali zao.

VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VIWE MACHO DHIDI YA WAVUNJA AMANI - DKT. MWIGULU
Studio Narration JAMBO FM

VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA VIWE MACHO DHIDI YA WAVUNJA AMA...

0:00 --:--

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuendelea kuwa macho dhidi ya vitendo vinavyolenga kuvuruga amani ya nchi huku akisisitiza kuwa Serikali itaendelea kusimamia usalama wa wananchi na mali zao.

Dkt. Mwigulu amesema hayo leo Jumamosi, Mei 23, 2026 alipozungumza na wananchi wa Manispaa ya Iringa katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Kichangani mkoani Iringa.

“Kuweni macho na njama za aina hii, shughulikeni na waovu wa aina hii. Mliweza lile la Kibiti, mliweza lile la Amboni na mambo mengine mengi mmeweza. Kuweni macho kuhakikisha michezo ya aina hiyo haifanikiwi huku mkihakikisha usalama wa raia wetu na mali zao unaendelea kulindwa,” amesema Dkt. Mwigulu.

Amesema amani ni msingi wa maendeleo ya Taifa na kwamba Watanzania wanapaswa kuendelea kulinda mshikamano wa kitaifa na kukataa vitendo vya uchochezi vinavyoweza kusababisha migawanyiko ya kisiasa, kidini au kijamii.

“Amani ni msingi wa maendeleo ya taifa letu. Kila mwananchi ana wajibu wa kuhakikisha nchi yetu inaendelea kuwa salama na yenye mshikamano,” amesema.

Aidha, Waziri Mkuu amesema zipo njama mbalimbali zinazolenga kuwagombanisha Watanzania kupitia siasa, dini na taarifa za upotoshaji huku akiwataka wananchi kuwa makini na watu wanaowachochea kufanya vitendo vinavyohatarisha usalama wa nchi.

“Tupuuze na wala tusiwe na ushirika na mtu anayekutuma kuvunja amani wakati yeye hayupo hapo na anajua yeye hataathirika,” amesema.

Kadhalika, Dkt. Mwigulu amesema baadhi ya matukio yanayoendelea kujitokeza nchini yakiwemo madai ya watu kujiteka au kushambuliwa yanapaswa kutazamwa kwa umakini mkubwa kwa kuwa baadhi yake yanaweza kuwa sehemu ya njama za kuwagawa Watanzania na kuichonganisha Serikali na wananchi wake.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.