Vyombo vya sheria Nchini, vimetakiwa kuchunguza kwa haraka na kwa haki vitisho na mashambulizi kwa Waandishi wa Habarii, kwani kutochukua hatua kwa wahusika kunadhohofisha demokrasia na haki ya wananchi kupata taarifa.
Wito huo, umetolewa jijini Dar es Salaam na na Mwenyekiti wa Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI), ambaye pia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Ernest Sungura kwenye maadhimisho ya awali ya Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Hali ya Kuadhibiwa kwa Uhalifu Dhidi ya Waandishi wa Habari Dniani.

Amesema, upo umuhimu wa uwazi, uwajibikaji na kuimarisha usalama wa Waandishi wa Habari, akiongeza kuwa, CoRI itaendelea kushirikiana na Serikali, Mamlaka za Udhibiti na Wadau kutetea uhuru wa habari na haki ya kupata taarifa.
Maadhimisho hayo kitaifa, yanatarajiwa kufanyika Mkoani Iringa Novemba 2, 2026, yakilenga kuimarisha uelewa kuhusu usalama wa Waandishi wa Habari Nchini.
Discussion
Reader comments
0 contributions