Skip to main content

VYAMA VYA USHIRIKA SHINYANGA VYATAKIWA KUWALIPA WAKULIMA KIDIJITALI

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

VYAMA VYA USHIRIKA SHINYANGA VYATAKIWA KUWALIPA WAKULIMA KIDIJITALI

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Wakulima wa zao la Pamba mkoani Shinyanga wametakiwa kufanya malipo yao wa kutumia mfumo wa kidigiti ili kuondokana na upotevu fedha unajitokeza kila msimu wa kilimo, kutokana na kutumia mfumo wa kulipa fedha mkononi (Cach).

Agizo hilo limetolewa leo Mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Shinyanga Julias Mtatiro akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, wakati wa mkutano wa nne wa Jukwaa la Maendeleo la Ushirikia mkoani humo.

“Dunia ya sasa siyo ya kutembea na mafurushi ya hela na kuwalipa wakulima,lazima tukubal mfuno wa kidigitali hivyo  ni vyema sasa kuanza kutumia mifumo ya kibenki hata mifumo ya simu,kila msimu kuna upotevu wa hela za wakulima,” amesema Mtatiro.

Kwa upande wake Mrajisi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Shinyanga,Kakozi Ibrahim, akiwasilisha taarifa ya hali ya ushirika mkoani Shinyanga amesema kuwa kuuza pamba kupita mfumo wa fedha tasilimu, umekuwa ukipoteza fedha nyingi na kutawataka kutumia mifumo ambao utaondoa changamo hiyo.

“Kiukweli na mimi niunge mkono suala hili la ulipaji wa hela kwa njia ya mkononi,imekuwa changamoto sana kwa wakulima wetu,mara kwa mara mana kumekuwa na upotevu wa fedha sana,kuuza kwa kutumia malipo ya mkononi kuna baadhi ya takwimu tunakuwa tunazikosa” Amesema Kakozi.

Awali, Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Mkoa wa ShinyangaEmanuel Nyambi, amesema kila mwaka wamekuwa wakipata hasara kutokana na vyama vya msingi kutumia mifumo wa kulipa wakulima kwa fedha tasilimu, na kuwaomba katika msimu wa kilimo watumie kwa njia ya simu ama benki.

“Mheshimiwa mgeni rasmi tunapendelea sana wakulima wetu walipwe kupitia benki kila mwaka tunapoteza mapato ya wakulima,hivyo ni vyema sasa kila chama cha msingi tuanze kuhamasishana kuhusu malipo kwa njia ya kidigitali ili kuzuia upotevu huu” Amesema Nyambi.

Naye, mkaguzi wa zao Pamba wilaya ya Kahama Emmanuel Kileo amesema kuwa bodi ya pamba imetoa muongozo mpya ambao, kila chama cha msingi cha wakulima wa zao hilo, wanapswa kulipwa fedha zao kwenye mfumo wa simu na benki.

“Mh Mgeni rasmi bodi ya pamba tayari imeweka muongozo mpya ambao kila chama cha msingi cha wakulima wa zao hilo wanapaswa kulipwa fedha zao kwa mfumo was imu na beki,hivyo ni matarajio yetu wakulima watazingatia suala hili” Amesema Kileo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.