Wakulima wa zao la Korosho Wilayani Uyui Mkoani Tabora, wamepewa viuatilifu vya zao hilo, ili kuwawezesha kuchochea kiwango cha uzalishaji na mavuno katika zao hilo la korosho.
Akizungumza katika uzinduzi wa ugawaji wa viuatilifu hivyo vya zao la Korosho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Shabani Katalambula amesema wakulima wazingatie maelekezo ya kitaalam kabla ya kutumia viatilifu hivyo.

Hata hivyo, Katalambula amewataka Wakulima kutumia viuatilifu hivyo kama vilivyokusudiwa kutumika katika zao la Korosho na si vinginevyo kwani viuatilifu hivyo vina ruzuku ya Serikali.
Aidha, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt.. Kija Maige amesema elimu iliyotolewa kuhusu matumizi yq Viuatilifu hivyo izingatiwe kwani ndiyo msingi wa matumizi mazuri na sahihi ya viutilifu hivyo.

Nao baadhi ya wakulima wamepongeza juhudi za Serikali katika kuhakikisha wakulima wanapata mazao bora ya Korosho.


Discussion
Reader comments
0 contributions