Kuna simulizi nyingi sana za eneo la Bermuda Triangle, ambazo ukizisikiliza ni lazima utaogopa ingawa ukweli wake ni tofauti na hadithi za mitandaoni.
Bermuda Triangle ni eneo la bahari kati ya Miami, Bermuda na Puerto Rico na hadithi zinasema ndege na meli hupotea hapo kimaajabu.

Eneo hilo ukubwa wake ni kama kilometa za mraba 1,300,000 baharini na hakuna mstari unaoonekana baharini kwa macho, ni ramani tu za wanadamu wamezichora, ili kuonesha eneo ambalo hadithi nyingi zilitokea.
Ukweli wa kisayansi:
1. Watafiti wanasema hakuna kitu cha ajabu kinachotokea hapo kuliko sehemu nyingine yoyote ya bahari.

Marekani na Uingereza waliwahi kufanya utafiti, wakadau bima za meli na ndege hazitozi pesa zaidi kupita Bermuda Triangle.
Wakasema, endapo ingekuwa hatari sana, bima zingekuwa ghali zaidi, lakini zina bei za kawaida kama bahari yoyote.

2. Sababu za kupotea:
(i) Hali ya hewa:
Ni eneo la dhoruba za ghafla na hurricane nyingi. Bahari inaweza kubadilika haraka.
(ii) Gulf Stream:
Ni mkondo wa bahari unaotembea kasi sana. Ukiacha mabaki ya ndege au meli, mkondo unayabeba haraka na kutoweka kabisa.

(iii) Makosa ya binadamu:
Ni moja ya njia zenye meli na ndege nyingi duniani. Kadiri foleni inavyokuwa nyingi, ndivyo ajali zinavyokuwa nyingi.
(iv) Dira ya sumaku (Magnetic Compass):
Katika eneo hilo dira huelekea Kaskazini ya kweli (True North) na Kaskazini ya sumaku (Magnetic North) tofauti kidogo, marubani wasiozoea huchanganyikiwa.

3. Uongo / Uchochezi.
Kesi maarufu kama Flight 19 (ndege 5 za jeshi la Marekani 1945) - uchunguzi ulionyesha kiongozi alipotea njia, mafuta yakaisha na wakaanguka baharini. Sio aliens.
Mwandishi Charles Berlitz ndiye aliyetengeneza umaarufu wa Bermuda Triangle mwaka 1974 kwa kitabu chake ili auze sana.

Hitimisho:
Hakuna shimo la ajabu, hakuna aliens, hakuna nguvu ya sumaku inayovuta vitu. Ni bahari kubwa, yenye dhoruba na watu wengi wanapita, kwa hiyo ajali zikitokea huonekana kama ni nyingi.
Ni kama ajali za barabarani, sio kwa sababu barabara imerogwa, hapana ila ni kwa sababu magari ni mengi na watu wanaendesha kwa kasi, unaoleta mfanano wa matukio ya BermudaTriangle.

Meli kubwa ya mizigo (kama USS Cyclops iliyopotea 1918 na watu 309) ikipigwa na dhoruba kali, au Ndege ya kijeshi ya zamani (kama Flight 19 - ndege 5 zilizopotea 1945) sababu ni shida ya sumaku ambayo marubani wengi walilalamika.
Mfano mwingine ni USS Cyclops (1918), Meli kubwa ya mizigo ya Marekani iliyobeba watu 306 na tani 10,800 za manganese, ilitoka Barbados kwenda Baltimore, ikasema "hali ya hewa ni nzuri" na ndipo ikapotea kabisa.

Hakuna mabaki yaliyopatikana hadi leo, ikawa hasara kubwa zaidi ya jeshi la maji la US kama ilivyo kwa Flight 19 (Dec 5, 1945) ambapo Ndege 5 za TBM Avenger zenye watu 14 zilitoka Fort Lauderdale kwa mazoezi.
Nazo zilipotea baada ya kusema "dira zimechanganyikiwa, na ndipo kila kitu kikaonekana cha ajabu.

Ndege ya uokoaji ya PBM Mariner yenye watu 13 iliyotumwa kuwatafuta nayo ilipotea pia. 9b57daa2
Qjali nyingine maarufu ni ile ya USS Proteus na USS Nereus (1941) - meli dada za Cyclops, zote zilipotea njia ile ile kama kwa SS Marine Sulphur Queen (1963) - tanker iliyoyeyuka, mabaki ya life preserver tu ndio yalipatikana.
Discussion
Reader comments
0 contributions