Skip to main content

VITA YA MALARIA: WANANCHI GEITA WAHIMIZWA UTOKOMEZAJI MAZALIA YA MBU

Na Ibrahim Rojala - Geita.

VITA YA MALARIA: WANANCHI GEITA WAHIMIZWA UTOKOMEZAJI MAZALIA YA MBU

Na Ibrahim Rojala - Geita.

Wananchi katika Halmashauri ya Manispaa ya Geita kwa kushirikiana na wenyeviti wa serikali za mitaa na watendaji wa mitaa hiyo, wametakiwa kushirikiana kutokomeza mazalia ya mbu kwa kuzingatia usafi wa mazingira, kuhakikisha hakuna madimbwi holela na kuendelea kuzingatia utekelezaji wa kampeni ya usafi wa mazingira maarufu kama  Hiyagulaga Geita inyoendelea kutekelezwa ndani ya Manispaa hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Geita, Hashim Komba ametoa rai hiyo Juni 30, 2026 wakati akizindua Kampeni ya Kinga dhidi ya ugonjwa wa Malaria ndani ya  Halmshauri ya Manispaa ya Geita kwa kutumia afua ya Unyunyizaji Viuadudu katika mazalia ya mbu, zoezi linalotarajiwa kutumia kiasi cha shilingi milioni 200 ambazo ni Fedha za uwajibikaji wa makampuni kwa jamii (CSR) kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGML) kwa mwaka 2025/2026.

Mkuu wa wilaya ya Geita, Hashim Komba.

“Bila afya hakuna maisha ya kawaida majumbani kwetu,bila afya hakuna uwekezaji,bila afya hakunaelimu,bila jambo lolote linaloweza kufanyika, na kama kuna jambo halivumiliki kwenye maisha ya mwanadamu basi ni maradhi”ameeleza DC Komba

Aidha,  Komba amewataka watendaji wa kila mtaa kutoa ushirikiano kwa wahudumu watakaopita katika mitaa yao kutekeleza zoezi hili na kueleza kwamba anapenda kuona maeneo yote yaliyolengwa na kampeni hii ndani ya Manispaa ya Geita yanafikiwa na kuuomba mgodi wa GGML kuitanua na kuifikisha kampeni hiyo katika halmashauri ya wilaya ya Geita ili kuendelea kuutokomeza ugonjwa huo hatari.

Mratibu wa Malaria Halmshauri ya Manispaa ya Geita, Mtashubirwa Nestory amesema kupitia kampeni hiyo, jumla ya mazalia ya mbu 1585 yaliyotambuliwa yenye mita za mraba 31,874 kutoka katika kata zote 13 za halmashauri ya Manispaa ya Geita mkoani Geita yanatarajiwa kunyunyuziwa viuadudu ambavyo ni pamoja na dawa ya ukoko yenye ujazo wa lita 150 pamoja na viuadudu lita 200.

Amebainisha kwamba Halmashauri ya Manispaa ya Geita ni miongoni mwa halmashauri zenye kiwango kikibwa cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria nchini ambapo kiwango cha maambukizi kwa mwaka 2025 kilikuwa asilimia 8.3, vifo vilivyotokana na ugonjwa huo vikiwa ni 15 sawa na asilimia 1.1.

Mratibu wa Malaria Halmshauri ya Manispaa ya Geita, Mtashubirwa Nestory.

“Ili kutekeleza zoezi hili kwa ufanisi,mafunzo yalitolewa kwaq wawezeshaji ambao walienda kuwezesha wasimamizi na wanyunyiziaji waliopata mafunzo na usimamizi ni wa watendaji wote wa Vijiji na mitaa kutoka kata zote,pia jumla ya wahudumu ngazi ya jamii 156 walipata mafunzo katika makundi manne,EPZ Bombambili,Kasamwa,Ihanamilo na Mtakuja,” ameeleza Mtashubirwa.

 Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa ya Geita, Dkt Fredrick  Mugarula amesema kati ya magonjwa 118 ya wagonjwa wa nje ugonjwa wa malaria unashika nafasi ya nne na tano ndani ya Manispaa hiyo akieleza kuwa katika kipindi cha mwaka 2025 takribani watu 10,845 waligundulika kuugua malaria na kusababisha madhara mbalimbali kama  vile vifo,maambukizi ya watoto walio tumboni na kupelekea baadhi ya watoto kuzaliwa wakiwa na viungo ambavyo havijakamilika.

“Kwenye ile idadi iliyosemwa ya wateja niliyoitaja ya 10,845 wastani wa gharama zilizotumika kutibu wateja hao zinacheza kati ya milioni 50 hadi milioni 100 inategemea na aina ya mgonjwa,umri wake kwahiyo dozi zinakuwa na utofauti kidogo,"

"Inategemea na complications au madhara mbalimbali aliyoyapata kutokana na malaria, kuna wengine wanapata na maambukizi ya bacteria kutokana na kuwa na malaria,kuna wengine inawapelekea hadi kuishiwa damu kwahiyo inabidi kuongezewa damu”ameeleza Dkt. Fredrick.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Geita, Dkt Fredrick  Mugarula.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Mgodi wa dhahabu wa Geita (GGML), Kaimu Mkurugenzi wa Mgodi huo, Dkt Kiva Mvungi amesema kwamba mgodi huo unaamini kuwa uchimbaji wa madini hauhusu kupata dhahabu pekee bali pia unahusu kuleta maendeleo ya kudumu kwa watu na jamii zinauozunguka mgodi huo ikijumuisha kusaidia mipango inayojumuisha kusaidia mipango inayoboresha afya,kuinua maisha ya wananchi na kuongeza ustawi wa jamii.

“Malaria bado ni moja ya changamoto kubwa kwa afya katika mkoa wetu,ingawa tumepiga hatua nzuri katika kupunguza maambukizi,bado familia nyingi zinaendelea kuathirika na ugonjwa unaoweza kuzuilika na kutibika.Kila mtu anayepata malaria anaathiri familia nzima,mtoto hukosa shule,mzazi hushindwa kufanya kazi na familia hupata mzigo wa gharama za matibabu,ndiyo maana kinga ni muhimu sana,” amebainisha Dkt. Kiva.

Kaimu Mkurugenzi wa Mgodi wa GGML, Dkt Kiva Mvungi.

Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wataalam watakaofika katika makazi yao kwaajili ya kunyunyiza dawa na kuwataka kushiriki katika kutoa  elimu,kuendelea kutumia vyandarua vyenye dawa kila siku na kuhakikisha wanaondoa mazalia ya mbu yanayozunguka makazi yao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.