Skip to main content

VIONGOZI WA TAASISI ZA UMMA WATAKIWA KULINDA MALI ZA SERIKALI

Na Daniel Gahu - Katavi.

VIONGOZI WA TAASISI ZA UMMA WATAKIWA KULINDA MALI ZA SERIKALI

Na Daniel Gahu - Katavi.

Mkurugenzi Msaidizi anayeshughulikia Sehemu ya Ajali na Fidia katika Idara ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Wizara ya Fedha, Dkt. Wenceslaus M. Sobayi, amewataka Maafisa Masuuli na viongozi wa taasisi za umma mkoani Katavi kuimarisha usimamizi wa mali za Serikali kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo iliyowekwa. Hatua hiyo itasaidia kuongeza ufanisi katika matumizi ya rasilimali za umma na kupunguza hoja za ukaguzi.

Akifungua mafunzo ya Usimamizi wa Mali za Umma yaliyofanyika katika Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Mkoa wa Katavi, Dkt. Sobayi amesema Serikali imeamua kuendelea kuwajengea uwezo viongozi na watendaji wakuu kutokana na changamoto zinazoendelea kujitokeza katika usimamizi wa mali za umma.

Amebainisha kuwa uhakiki uliofanywa na Wizara ya Fedha katika taasisi mbalimbali za umma kwa miaka ya fedha 2023/24 hadi 2025/26 umebaini mapungufu kadhaa, ikiwemo kutokuwepo kwa nyaraka muhimu za umiliki wa mali, kutoingizwa kwa taarifa za mali katika Mfumo wa Serikali wa Usimamizi wa Mali (GAMIS), kutowiana kwa taarifa za mali pamoja na uwepo wa mali chakavu, sinzia na ziada.

“Mapungufu haya yanaifanya Serikali kuendelea kubeba gharama kubwa za ununuzi na matengenezo ya mali, huku yakichochea hoja za ukaguzi kutoka kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),” amesema Dkt. Sobayi.

Aidha, amesisitiza kuwa Maafisa Masuuli wana wajibu wa kuhakikisha mali zote za umma zinaingizwa kwenye mfumo wa GAMIS, zinatunzwa ipasavyo, zinatumika kwa manufaa yaliyokusudiwa na taarifa za ajali, upotevu au hasara za mali zinawasilishwa kwa wakati kwa mamlaka husika.

Akizungumza kwa niaba ya washiriki, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Bi. Shamim Mwariko, ameipongeza Wizara ya Fedha kwa kuandaa mafunzo hayo yenye manufaa makubwa katika utekelezaji wa majukumu yao.

Pia ameiomba Wizara kuendelea kutoa mafunzo ya mara kwa mara, hususan kuhusu matumizi ya Mfumo wa GAMIS, ili kuongeza ufanisi wa kazi, kuimarisha uwajibikaji na kuhakikisha usimamizi bora wa mali za umma.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.