Skip to main content

VIONGOZI WA CCM GEITA WAHIMIZWA UBUNIFU MIRADI ITAKAYOJIENDESHA

Na Ibrahim Rojala - Geita.

VIONGOZI WA CCM GEITA WAHIMIZWA UBUNIFU MIRADI ITAKAYOJIENDESHA

Na Ibrahim Rojala - Geita.

Katibu wa NEC-Organaizesheni, Issa Ussi Haji (Gavu)  ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Geita, amewataka viongozi wa chama hicho kutengeneza miradi mingi itakakayosimama na kujiendesha, ili fedha zitakazopatikana zitumike kuendesha shughuli za ziasa za chama hicho badala ya kuwategemea viongozi kufadhili shughuli hizo.

Ameeleza hayo Aprili 18, 2026 akiwa mkoani Geita katika Mkutano Mkuu wa kawaida wa chama hicho ulioketi katika eneo la ujenzi wa ofisi za chama hicho Magogo, Manispaa ya Geita kwa lengo la kupokea taarifa za utekelezaji wa ilani ya CCM ndani ya mkoa wa Geita kwa kipindi cha miaka minne (2022-2026).

Katibu wa NEC-Organaizesheni, Issa Ussi Haji (Gavu)  ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Geita.

“Kuna nyakati mnashindwa kufanya ziara hasa  ngazi za chini kwa maana kwamba kila kinachofanywa chini lazima kitegemee diwani na viongozi wa kuchaguliwa, njia pekee ya kondokana na hilo ni kutengeneza miradi mingi, itakayosimama,itakayojiendesha ili kitakachopatikana kiweze kufanya shughuli za siasa na ziara kwenye maeneo yenu,” ameeleza Gavu

Awali, akiwasilisha  taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM ndani ya mkoa wa Geita katika kipindi cha miaka minne(2022-2026), Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema kuwa Pato la mkoa wa huo limeongezeka kutoka trilioni 7.7 katika kipindi cha mwaka 2022 hadi kufikia kiasi cha shilingi trilioni 9.3 mwaka 2026 wakati wastani wa pato la mtu mmoja mmoja kwa mwaka likifika kiasi cha shilingi milioni 2.8.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Geita, Nicholaus Kasendamila.

Kwa upande wa sekta ya madini ameelezea kuwa uzalishaji wa dhahabu kwa mwaka 2022 ulikuwa tani 18.2 kabla ya kuongezeka hadi kufikia tani 27.4 mwaka 2026 hali iliyochochewa na utwaaji wa leseni zilizokuwa hazitumiki katika uzalishaji na kuwakabidhi wachimbaji wadogo.

Ameelezea hatua hiyo pia imechochea kuongezeka kwa mapato ya halmashauri za mkoa huo kutoka bilioni 6.1 hadi bilioni 10.5 kutoka katika mapato yatokanayo na madini.

Sehemu ya wanaCCM waliohudhuria Mkutano Mkuu wa kawaida.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Geita, Nicholaus Kasendamila amesema ndani ya kipindi cha miaka minne chama hicho kimefanikiwa kufanya ziara katika kila kata ndani ya kila mwaka,kufanikisha ujenzi wa ofisi ya mkoa ya chama pamoja na kufanikisha kusimamia Uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Akizungumza katika mkutano huo, Naibu waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko amepongeza kufanyika kwa mkutano huo akipeleza kwamba wabunge wa mkoa wa Geita wataendelea kuwa watiifu kwa chama na kutoa ushirikiano wilayani akiwaomba wananchi kuendelea kuwatengeneza wabunge wao kuwa bora.

Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko.

“Mnakuwa na wabunge wanaelea, lakini akikosea waiteni, wazee wapo hapa mwambieni wewe kwa njia unayokwenda sio sawa,na  ningetamani sisi wabunge tuwe watu wa kuwaunganisha watu,kuwasukuma watu kwenye uelekeo mmoja, aiwepo wa huyu wa huyu wawepo wana CCM wa mkoa wa Geita wenye nia moja ya kuijenga Geita ili Geita baada ya miaka 50 watoto wa watoto wetu waikute Geita iliyo bora kuliko tuliyoikuta,” amesema Dkt Biteko.

Jengo la CCM linaloendelea kujengwa.

Naye Mwenyekiti wa Wachimbaji Madini mkoa wa Geita (GEREMA) na mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Geita, Titus Charles Kabuo amesema ndani ya kipindi cha miaka minne,serikali imefanya mambo makubwa katika sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na kutengeneza mazingira mazuri ya uwekezaji na ushirikiano kati ya wawekezaji na serikali.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.