Skip to main content

VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA, VIKUNDI VYA ULINZI NA WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTUNZA AMANI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, (DCP) Wilbrod Mutafungwa, amewataka viongozi wa mitaa kushirikiana kwa na Jeshi la Polisi katika kutambua na kudhibiti vitendo vya uhalifu, akisisitiza kuwa jukumu la kuzuia uhalifu ni la kila mwananchi.

VIONGOZI SERIKALI ZA MITAA, VIKUNDI VYA ULINZI NA WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTUNZA AMANI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, (DCP) Wilbrod Mutafungwa, amewataka viongozi wa mitaa kushirikiana kwa na Jeshi la Polisi katika kutambua na kudhibiti vitendo vya uhalifu, akisisitiza kuwa jukumu la kuzuia uhalifu ni la kila mwananchi.

DCP Mutafungwa ametoa wito huo Juni 18, 2026 katika Uwanja wa Polisi Mabatini wakati wa kikao kilichowakutanisha viongozi mbalimbali wakiwemo watendaji wa kata na mitaa, wenyeviti, wazee maarufu, viongozi wa dini pamoja na vikundi vya ulinzi shirikishi.

Amesema Jeshi la Polisi limehakikisha huduma za Polisi Kata zinapatikana katika kata zote ili kuimarisha utoaji wa elimu kwa jamii na ushirikiano katika kutekeleza mikakati ya kuzuia uhalifu.

Akizungumza katika kikao hicho, DCP Mutafungwa amewataka viongozi hao kuwafahamu wakazi na wageni wanaoingia na kutoka katika maeneo yao na kutoa taarifa kwa mamlaka husika wanapobaini watu wanaotiliwa shaka au wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa.

" Jeshi la Polisi limehakisha kwamba elimu ya  uhalifu inafikiwa kwa jamii nzima kupitia Polisi kata ambao wameletwa katika Kata zote, hivyo kuwatumia katika mambo mbalimbali yanayohusu mkakati ya uzuiya uhalifu kwani wajibu wa kuzuiya uhalifu si wa Jeshi la Polisi peke yake bali ni wajibu wa kila mmoja wetu kuhakikisha maeneo yetu yanabaki kuwa salama," alisema.

Aidha, amewataka waganga wa jadi kutoa ushauri sahihi kwa wananchi wanaowafuata kwa matatizo ya kiafya kwa kuwaelekeza hospitalini pale inapobidi badala ya kuendelea kuwahudumia kwa huduma wasizoweza kuzitoa.

Amesema, "Mtu anaumwa mpe ushauri aende Hospitali, uisendelee kuchukuwa hela, hospitali za rufaa zipo, tuwaelekeze watu wakapate tiba, wewe tibu kile unachokiweza tu."

Kwa upande wao, baadhi ya viongozi walioshiriki kikao hicho wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa juhudi zake za kuimarisha usalama na kupambana na vitendo vya uhalifu katika Mkoa wa Mwanza.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.