Na Afarah Suleiman, Mbulu - Manyara.
Viongozi wa ngazi mbalimbali wilayani Mbulu mkoani Manyara, wametakiwa kuweka kipaumbele katika usimamizi wa masuala ya lishe kwenye taasisi za elimu, ili kupunguza tatizo la udumavu na utapiamlo kwa watoto.
Agizo hilo, limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Michael Semindu baada ya kuhitimishwa kwa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya hiyo,ambapo amesisitiza umuhimu wa viongozi kushirikiana katika kuhakikisha watoto wanapata lishe bora shuleni na nyumbani kwa lengo la kuboresha afya na maendeleo yao.

Naye Afisa Lishe toka Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Jacline Davidi Amesema wanaendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora na matumizi ya vyakula vyenye virutubisho muhimu ili kukabiliana na tatizo la udumavu na utapiamlo….
Kwa upande wao, Maafisa Elimu Wilayani humo, wamesema wataendelea kusimamia utekelezaji wa mipango ya lishe mashuleni sambamba na kuhamasisha wazazi na walezi kushiriki kikamilifu katika kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula bora wanapokuwa shuleni.

Nao Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, wameahidi kushirikiana na wataalamu wa afya na elimu katika kuhakikisha mikakati ya kuboresha lishe inatekelezwa kwa ufanisi katika maeneo yao.





Discussion
Reader comments
0 contributions