Mvutano mkali na uhasama umeibuka Kati ya Serikali ya Ethiopia inayoongozwa na Aby Ahmed Ali na Eritrea, baada ya Vikosi kadhaa vya jeshi la Eritrea kuingia kaskazini mwa Ethiopia kuelekea mji wa Tigray, ambako vuguvugu la mapigano makali linaendelea kati ya jeshi la Serikali na vikosi vya waasi vya upinzani.

Vikosi vya Eritrea vimeingia nchini Ethiopia wakati ambapo mvutano mkali ukiendelea kushika kasi kati ya Serikali na Chama cha upinzani cha TPLF, kinachodhibiti eneo la Tigray.
Duru kutoka Barani Africa zinaeleza kuwa uhasama kati ya pande hizo unazidi kuongezeka kutokana na tuhuma mseto baina yao, kukiuka kile kilichoelezwa mkataba wa mwaka 2022 uliotamatisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya takribani miaka miwili mfululizo.

Kuwasili kwa vikosi vya Eritrea mjini Tigray kunatajwa kuongeza uhasama kati ya Ethiopia na nchi hiyo ambayo hapo awali walikuwa na ushirika wa karibu hasa katika vita vya 2020 dhidi ya TPLF, uhusiano ulioyumnba baada ya Abiy Ahmed Ali Waziri Mkuu wa Ethiopia, kufikia bandari za Eritrea bahari ya Shamu.
Discussion
Reader comments
0 contributions