Skip to main content

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA KUJIKWAMUA KIUCHUMI KIGOMA

Vijana kutoka Wilaya za Kasulu na Kibondo Mkoani Kigoma wametakiwa kutumia fursa zinazopatikana katika maeneo yao ili kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA KUJIKWAMUA KIUCHUMI KIGOMA
Studio Narration JAMBO FM

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA KUJIKWAMUA KIUCHUMI KIGOMA

0:00 --:--

Vijana kutoka Wilaya za Kasulu na Kibondo Mkoani Kigoma wametakiwa kutumia fursa zinazopatikana katika maeneo yao ili kujikwamua kiuchumi na kuboresha maisha yao.

Hayo yameelezwa na Katibu tawala wa wilaya ya Kasulu, Bi. Theresia Mtelewe, wakati akimuwakilisha mkuu wa wilaya hiyo kwenye mdahalo unao waweka pamoja vijana katika kujadili changamoto na fursa ili kuwafanya kuwa sehemu ya maendeleo katika mkoa wao.

Baadhi ya vijana walioshiriki mdahalo huo, Picha na Tryphone Odace

Amesema ni muhimu kwa vijana kuzitambua na kuzichangamkia fursa hizo ili kujipatia kipato na kushiriki kikamilifu katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii, licha ya changamoto ya upatikanaji wa ajira.

Mratibu wa Jukwaa la Vijana kutoka Shirika la ActionAid, Arif Fazel, amesema mdahalo huo umelenga kuwaunganisha vijana ili kujadili changamoto zinazowakabili, kutambua fursa zilizopo na kupata uelewa wa namna ya kuzitumia kwa ajili ya kujiletea maendeleo.

Mratibu wa jukwa la vijana kutoka shirika la Actionaid, Arif Fazel, Picha na Tryphone Odace

Naye Afisa Biashara wa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Mikamba Bakari, amezungumzia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana katika halmashauri hiyo, akitaja sekta ya kilimo kuwa miongoni mwa maeneo yenye fursa kubwa kwa vijana kujipatia kipato.

Afisa biashara halmashauri ya Wilaya Kasulu Mikamba Bakari, Picha na Tryphone Odace

Baadhi ya vijana walioshiriki katika mdahalo huo wamesema wamejifunza mambo mbalimbali yatakayowasaidia kutambua fursa zilizopo katika maeneo yao na kuzitumia kwa ufanisi ili kujikwamua kiuchumi na kufikia malengo yao ya maendeleo.

Jumla ya Vijana 150 kutoka wilaya za Kasulu na Kibondo wamejitikeza kushiriki mdahalo huo uliofanyikia Kasulu Mjini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.