Skip to main content

VIJANA WANA WAJIBU KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UJENZI WA TAIFA - DC MWENDA

Na Saulo Stephen - Singida.

VIJANA WANA WAJIBU KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA UJENZI WA TAIFA - DC MWENDA

Na Saulo Stephen - Singida.

Imeelezwa kuwa vijana wana wajibu mkubwa wa kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa, akisisitiza kuwa wao ndiyo nguvu kazi ya nchi na kwamba utekelezaji wa miradi ya maendeleo unategemea mchango na ushiriki wao.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Alhaji Suleiman Yusuph Mwenda, wakati akizindua rasmi Jukwaa la Vijana la Halmashauri ya Wilaya ya Iramba maarufu kama Vijana Platform, lililoandaliwa kuelekea mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Wilayani Iramba yanayotarajiwa kufanyika Julai 24, 2026.

Akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika katika Ukumbi Mkubwa wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, DC Mwenda amewataka vijana kuwa wazalendo kwa kuipenda na kuthamini nchi yao, huku wakitambua na kujivunia mafanikio yanayopatikana katika sekta mbalimbali nchini.

Amesema vijana wanapaswa kutumia nafasi yao kama nguvu kazi ya Taifa kwa kushiriki katika shughuli za maendeleo, kuibua fursa zilizopo na kuhakikisha wanakuwa sehemu ya suluhisho katika changamoto mbalimbali zinazolikabili taifa.

“Ipendeni nchi yenu, wapendeni viongozi wenu, hatuna nchi nyingine zaidi ya hii Tanzania,” amesema DC Mwenda.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewahimiza vijana kuwa na maono makubwa ya maisha, kuwekeza katika elimu na ujuzi ili kujijengea uwezo wa kujitegemea na kuchangia maendeleo ya jamii inayowazunguka.

Katika kongamano hilo la vijana, washiriki wamepatiwa elimu kupitia mada mbalimbali zilizolenga kuwajengea uwezo, kuimarisha uzalendo na maadili mema, pamoja na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.

Miongoni mwa mada zilizowasilishwa ni pamoja na uzalendo na uraia, amani na mshikamano wa jamii, mapambano dhidi ya dawa za kulevya na rushwa, pamoja na namna ya kutumia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika maeneo yao.

Uzinduzi wa Jukwaa hilo ni sehemu ya maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru Wilayani Iramba, huku ukiwa na lengo la kuwakutanisha vijana, kuwajengea uelewa na kuwaandaa kushiriki katika safari ya maendeleo ya Taifa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.