Skip to main content

VIJANA WAHIMIZWA KUJIANDAA KABLA YA KUSHIRIKI MAAMUZI YA KITAIFA

Mjadala wa kitaifa wa ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi na vijana katika ngazi za maamuzi kwa maendeleo endelevu umefanyika Leo hapa jijini Mwanza chini ya Doyodo Tanzania Ambapo mwasilishaji Deus Kibamba amesema kua Mjadala huo umeangazia umuhimu wa vijana kuzingatia vitu vya msingi kabla ya kushiriki kikamilifu katika maamuzi ya serikali.

VIJANA WAHIMIZWA KUJIANDAA KABLA YA KUSHIRIKI MAAMUZI YA KITAIFA

Mjadala wa kitaifa wa ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi na vijana katika ngazi za maamuzi kwa maendeleo endelevu umefanyika Leo hapa jijini Mwanza chini ya Doyodo Tanzania Ambapo mwasilishaji Deus Kibamba amesema kua Mjadala huo umeangazia umuhimu wa vijana kuzingatia vitu vya msingi kabla ya kushiriki kikamilifu katika maamuzi ya serikali.

Miongoni mwa mambo yaliyotajwa ni kuwa na kitambulisho cha mpiga kura na kitambulisho cha NIDA, ambavyo vinamwezesha kijana kushiriki katika uchaguzi na michakato mingine ya kidemokrasia bila kikwazo.

Aidha, Geline Alfred Fuko  amewahimiza vijana kujifunza na kufanya utafiti wa kina kuhusu masuala yanayowagusa Katika ushiriki wenye tija unahitaji ufahamu wa kutosha ili anapofika wakati wa kuibua mjadala au kutoa mchango, awe na hoja zenye uzito na si kelele tu.

Maarifa haya yanamwezesha kijana kutoa mchango wenye maana na kuaminika, hasa katika masuala yanayohusu Katiba ya nchi.

Sehemu nyingine iliyosisitizwa ni umuhimu wa kufahamu na kufuatisha Katiba ya nchi kwani viongozi wengi hawafuatishi Katiba kama inavyopaswa.

Hali hii imeonekana kuwa changamoto kubwa ambayo kizazi cha sasa cha vijana kinapaswa kuchukua jukumu la kuirekebisha kupitia ushiriki makini na uwajibikaji. 

Ally Kashimiri naye amewataka vijana kutumia fursa ya mitandao ya kijamii, akibainisha kuwa kwa sasa mitandao ina msukumo mkubwa na ushawishi wa kumfunza na kumjenga kijana ili kubata kesho iliyo bora.

Alisisitiza kuwa vijana wanapaswa kubadilisha matumizi ya mitandao kutoka burudani tu hadi kuwa chombo cha kujifunza, kushawishi maamuzi, na kujenga uelewa wa kisiasa na kijamii.

Kwa ujumla, ujumbe wa mjadala ni wazi: ushiriki wa vijana katika maamuzi ya taifa hauwezi kuwa na maana kama hauna msingi wa elimu, utafiti, na uelewa wa sheria.

Kijana mwenye ufahamu, nyaraka sahihi, na matumizi sahihi ya mitandao ndiye atakayeweza kuleta mabadiliko halisi na kuchangia katika kujenga maendeleo endelevu nchini.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.