Skip to main content

VIFO VYA MAMA NA MTOTO: WAHUDUMU WA AFYA SINGIDA WAPEWA MAFUNZO MATUMIZI NYENZO MPYA LCG

Na Saulo Stephen - Singida.

VIFO VYA MAMA NA MTOTO: WAHUDUMU WA AFYA SINGIDA WAPEWA MAFUNZO MATUMIZI NYENZO MPYA LCG

Na Saulo Stephen - Singida.

Katika kuhakikisha huduma ya afya ya mama na mtoto mkoani Singida inayolenga kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga inaimarishwa, watoa huduma wa afya wamepokea mafunzo maalum ya matumizi ya nyenzo mpya ya Labour Care Guide (LCG) ambayo inalenga kuboresha ufuatiliaji wa uchungu wa uzazi na kuongeza uwezo wa kufanya maamuzi ya haraka yanayookoa maisha.

Akifungua mafunzo hayo, Mganga Mkuu Mkoa wa Singida, Dkt. Jesca Lebba, katika Hospitali ya Manispaa ya Singida Juni 24,2026, ameagiza watoa huduma wote kutumia kikamilifu LCG katika vituo vyote vya afya, akisisitiza kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kupunguza kwa kasi vifo vya mama na mtoto kupitia ufuatiliaji wa kitaalamu na wa karibu zaidi wa mama mjamzito.

Dkt. Lebba amesema uwekezaji mkubwa wa serikali katika sekta ya afya miundombinu, vifaa tiba na rasilimali watu unapaswa kuendana na matumizi sahihi ya zana za kisasa kama LCG. Amesema wazi kuwa kila mama mjamzito anayeingia chumba cha kujifungulia lazima afuatiliwe kwa umakini ili kubaini viashiria hatarishi mapema na kuchukua hatua bila kuchelewa.

Ameelekeza kuwa kila mtoa huduma anayeshiriki mafunzo haya awe “mtaalamu chachu” wa kusambaza ujuzi huo kwenye vituo vyao, ili Mkoa mzima wa Singida utumie LCG kama mfumo wa kawaida wa ufuatiliaji wa leba. Amesisitiza kuwa huduma duni za kliniki za wajawazito na uzembe katika vipimo vya msingi vinapaswa kukomeshwa mara moja, akisema uwajibikaji sasa ni kipimo cha maisha.

Aidha, Dkt. Lebba amesisitiza kuwa hakuna mama anayepaswa kupoteza maisha wakati akipokea huduma ya afya, akielekeza kuwa kila kituo kitawajibika moja kwa moja kwenye takwimu za vifo vya mama na watoto. 

Naye Mratibu wa Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto Mkoa wa Singida, Bi. Caroline Minja, amesema mkoa umeacha rasmi matumizi ya mfumo wa zamani wa partograph na sasa umeanza kutumia.

Mafunzo haya yameweka mwelekeo mpya katika huduma za afya ya uzazi mkoani Singida, ambapo LCG sasa inaonekana kama nyenzo muhimu ya kupunguza vifo vya mama na watoto, huku msisitizo ukiwa ni uwajibikaji, weledi na ufuatiliaji wa karibu katika kila hatua ya huduma za afya ya mama mjamzito.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.