Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi amemwelekeza Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillius Wambura, kutotoa vibali vya mikutano ya hadhara katika kipindi hiki, akieleza kuwa hatua hiyo inalenga kulinda usalama wa wananchi kutokana na kuwepo kwa viashiria vya matishio ya amani.
Waziri Katambi ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa pia Serikali imeanza kuchukua hatua dhidi ya baa, sehemu za starehe na biashara nyingine zinazokiuka taratibu za uendeshaji, kwa kuzizuia kuendelea na shughuli zake katika kipindi hiki hadi zitakapokidhi matakwa ya sheria.

Amesema, maeneo yote ya burudani yanayofanya kazi usiku yatafanyiwa tathmini ya kiusalama, na iwapo uchunguzi utabaini kuwa yanahatarisha usalama wa wananchi au yanahusishwa na vitendo vinavyoweza kuvuruga amani, yatafungiwa mara moja.
Discussion
Reader comments
0 contributions