Baada ya wiki ya chanjo kuzinduliwa Halmashauri ya jiji la Mwanza imetoa chanjo ya polio kwa watoto chi ya miaka 10, huku Afisa Tawala wa Wilaya ya Nyamagana, Magreth John amesema kua viashiria vya uwepo wa ugonjwa wa polio vimeonekana katika maeneo ya kanda ya ziwa huku mkoa wa mwaza ukiwa ni miongoni mwa mikoa saba ya Mwanzo kupata huduma ya chanjo ya polio
Kupitia kampeni hiyo, amewataka wazazi kuwapeleka watoto wao kupata chanjo, ikizingatiwa ni kipindi cha likizo, hivyo watapita kila nyumba kuhahkikisha wakazi wa jiji la Mwanza wanakua salama dhidi ya maradhi ya polio.

Naye Gipson Simbuya, Mfamasia wa jiji la Mwanza amesema kama ikitokea virusi hivyo vimetokea watoto ninlqzima wakingwe kwani wao ndio waathirika wakubwa na kinga yao ya mwili bado haijakomaa, hivyo unaweza kusababisha ulemavu wa kudumu ama kifo.
John Mbira ni Diwani wa Kata ya Mkolani, yeye amesema kua wazazi wengi sada ni waelewa juu ya mambo haya ya chanjo kwani kujitokeza kwao kwa wingi, inaonyesha dhahiri kuwa wamelenga kulinda afya ya mtoto
Discussion
Reader comments
0 contributions