Skip to main content

UZIO WASABABISHA WIZI MALI ZA WATOTO YATIMA KAHAMA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

UZIO WASABABISHA WIZI MALI ZA WATOTO YATIMA KAHAMA

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Ukosefu wa uzio katika kituo cha watoto yatima cha Kahama Peace orphanage  center kilichopo Mtaa wa bukondamoyo kata ya Muhungula wilayani Kahama mkoani Shinyanga umesababisha wizi wa mali za watoto hao ikiwemo Ng’ombe wa maziwa,kuku na magodoro.

Hayo yamebaishwa na Meneja wa kituo hicho Abubakar Gwandi wakati akisoma risala mbele ya mgeni rasmi katika sherehe ya miaka 12 ya mafanikio ya makao ya watoto yatima wa kituo hicho.

Amesema licha kuwa na ulinzi katika kituo hicho lakini kutokana na ukubwa wa eneo  na sehemu kubwa kuwa wazi wanashindwa kumudu maeneo yote hali iliyopelekea mali hizo kuibiwa.

“Ndugu mgeni rasmi Pamoja na mafanikio hayo niliyoyaeleza lakini kituo chetu kinakabiliwa na ukosefu wa uzio hali iliyosababisha mali za watoto yatima kuibiwa ikiwa ni Pamoja na Ng’ombe wa maziwa,kuku Pamoja na magodoro,” alisema Gwandi.

Katika hatua nyingine Gwandi amesema kuwa changamoto nyingine wanayokutana nayo ni pamoja na ukosefu wa chakula kwani kituo kina watoto zaidi ya 90 ambao wanahitaji kupata chakula asubuhi,mchana na jioni.

“Ndugu mgeni rasmi Changamoto nyingine tunayokumbana nayo ni upungufu wa chakula kituo chetu kina watoto zaidi ya 90 ambao wote wanahitaji kula milo mitatu kwa siku, lakini wakati mwingine chakula hakitoshelezi hivyo tunaomba wadau wa maendeleo watusaidie chakula ili watoto hawa wapate chakula muda wote,” aliongeza Gwandi.

 Kwa upande wake Mkurugenzi wa kituo hicho Bi Halima Hamza amewashukuru wananchi wa manispaa ya Kahama na taasisi za serikali kwa ushirikiano  mkubwa wanaoutua katika kituo hicho kwa lengo la kuwasaidia watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu.

“Kwakweli sina cha kusema niwashukuru sana wananchi wa manispaa ya Kahama kwa mchango mkubwa wa kuwasaidia watoto hawa,taasisi za serikali ikiwemo jeshi la polisi na ofisi ya mkurugenzi kwa kujitoa kuhakikisha watoto wanaishi katika mazingira mazuri,” alisema Bi Halima.

Kwa upande wake Mgeni rasmi wa tukio hilo Mdau wa Maendeleo Sultani Mitimingi ametoa wito kwa wananchi kujitoa na kulea watoto yatima kwani ni ibada inayompendeza Mungu na kwamba watoto hao ni wetu sote hivyo ni jukumu letu kuwasaidia na ametoa mifuko 100 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa uzio huo.

“Niwaombe ndugu zangu tuzidi kujitoa kwa ajili ya watoto hawa,Kwani vitabu vya madhehebu yote vinatusihi kuwalea watoto yatima kwani ni sadaka kwa Mwenyezi Mungu,kama umepata nafasi toa kwa ajili ya watoto yatima na wajane Pamoja na watu wasiojiweza,” amesema Mitimingi. 

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.