Skip to main content

UZIO WA KILOMETA 104 KUJENGWA PORI LA AKIBA MASWA

Na Gideon Gregory - Dodoma.

UZIO WA KILOMETA 104 KUJENGWA PORI LA AKIBA MASWA

Na Gideon Gregory  - Dodoma.

Serikali kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi katika mwaka 2026/27 inatarajia kujenga uzio wa umeme (electrified fence) wenye urefu wa kilomita 104 kwenye mpaka wa hifadhi ya Pori la Akiba Maswa kwa upande wa magharibi unaopakana na makazi ya wananchi katika Wilaya za Meatu, Itilima na Bariadi. 

Hayo yamebainishwa leo Aprili 14,2026 Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Hamad Chande wakati akijibu swali la Mbunge wa Meatu Mhe. Salum Khamis Salum, aliyehoji Serikali ina mpango gani wa haraka na wa kudumu wa kuzuia tembo kuvamia vijiji Meatu na kuwarudisha hifadhini.

Chande amesema uzio huo utawezesha kudhibiti tembo kutoka nje ya hifadhi na kuongeza kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za haraka katika kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu hususani tembo kwenye maeneo mbalimbali nchini ikiwemo vijiji vya Wilaya ya Meatu. 

"Hatua hizo ni pamoja na kujenga vituo vinne (4) vya Askari wa kudhibiti wanyamapori wakali na waharibifu na kuviwezesha rasilimali watu pamoja na vitendea kazi muhimu ambapo kupitia vituo hivyo, kati ya mwezi Julai 2025 hadi Machi 2026 doria zilifanyika na kuwezesha kudhibiti matukio 352 katika Wilaya ya Meatu," amesema. 

Aidha, amwelekeza Kamishna Mkuu wa TAWA na  TANAPA kwa kushirikiana na halmashauri zote nchini waende kuondoa wanyama hao walioko katika makazi ya watu na mashamba yao.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.