Skip to main content

UZALISHAJI WA MAZAO WENYE TIJA: TANGANYIKA WAPOKEA KIFAA MAALUM CHA KUPIMA UDONGO

Na Daniel Gahu - Katavi.

UZALISHAJI WA MAZAO WENYE TIJA: TANGANYIKA WAPOKEA KIFAA MAALUM CHA KUPIMA UDONGO

Na Daniel Gahu - Katavi.

Katika kuimarisha sekta ya kilimo kupitia matumizi ya sayansi na teknolojia, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika imepokea kifaa maalumu cha kisasa cha kupimia afya ya udongo (Soil Scanner) kilichotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kupatikana kwa kifaa hicho kunalenga kuboresha huduma za upimaji wa udongo kwa wakulima, ili kuwawezesha kupata taarifa sahihi kuhusu hali ya udongo katika maeneo yao na hivyo kufanya maamuzi bora ya uzalishaji wa mazao.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka halmashauri hiyo, kifaa hicho tayari kimeonesha matokeo chanya ambapo kimewezesha kupimwa jumla ya sampuli 1,400 za udongo katika mzunguko mmoja wa upimaji. Hatua hiyo ni mafanikio makubwa katika juhudi za kuhakikisha wakulima wanapata huduma za uchunguzi wa udongo kwa ufanisi na kwa wakati.

Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika sasa inatarajia kuongeza kasi ya upimaji wa sampuli za udongo baada ya kuwa na jumla ya vifaa viwili vya kupimia udongo. Kuongezeka kwa vifaa hivyo kutasaidia kupunguza muda wa kusubiri huduma, kuongeza idadi ya sampuli zinazopimwa, pamoja na kuwafikia wakulima wengi zaidi katika maeneo mbalimbali ya halmashauri.

Soil Fertility Analysis. Female agronomist taking soil sample. Environmental protection, organic soil certification, research, close up

Wataalamu wa kilimo wanaeleza kuwa upimaji wa udongo ni hatua muhimu inayomwezesha mkulima kufahamu kiwango cha rutuba, virutubisho vinavyopatikana pamoja na mahitaji ya udongo wake. Taarifa hizo humsaidia kuchagua mbolea sahihi, kupanga matumizi bora ya virutubisho na kuongeza tija ya uzalishaji wa mazao.

Uwekezaji huu wa Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais unaonesha dhamira ya kuendelea kuimarisha kilimo chenye tija kwa kutumia teknolojia za kisasa, sambamba na kuongeza usalama wa chakula na kuinua kipato cha wakulima.

Ni matarajio ya Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika kuwa huduma hii itaendelea kuwafikia wakulima wengi zaidi, hivyo kuchochea ongezeko la uzalishaji wa mazao na kuchangia maendeleo ya sekta ya kilimo katika wilaya hiyo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.