Skip to main content

UWEKEZAJI KWA VIJANA, WANAWAKE NI MSINGI WA AMANI NA MAENDELEO - NDEJEMBI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amesema uwekezaji kwa wanawake na vijana kupitia elimu, mafunzo, ujuzi na fursa za kiuchumi ni msingi muhimu wa kujenga amani na maendeleo endelevu katika ukanda wa Maziwa Makuu.

UWEKEZAJI KWA VIJANA, WANAWAKE NI MSINGI WA AMANI NA MAENDELEO - NDEJEMBI
Studio Narration JAMBO FM

UWEKEZAJI KWA VIJANA, WANAWAKE NI MSINGI WA AMANI NA MAENDEL...

0:00 --:--

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, amesema uwekezaji kwa wanawake na vijana kupitia elimu, mafunzo, ujuzi na fursa za kiuchumi ni msingi muhimu wa kujenga amani na maendeleo endelevu katika ukanda wa Maziwa Makuu.

Amesema hayo leo Novemba 2, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mkutano wa wabunge wanawake wa nchi za ukanda wa Maziwa Makuu, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Ndejembi amesema wanawake na vijana wanapaswa kupewa nafasi ya kushiriki katika shughuli za ujenzi wa amani na kuandaliwa kuwa viongozi wenye maarifa, uwezo, uzalendo na uwajibikaji.

Amesisitiza kuwa wanawake hawapaswi kutazamwa kama wahanga wa migogoro pekee, bali pia viongozi, wapatanishi na wadau muhimu katika kujenga amani na kurejesha matumaini kwa jamii zilizoathirika.

Amesema ushiriki wenye maana wa wanawake ni sehemu ya suluhu, msingi wa maamuzi jumuishi na nyenzo muhimu ya kujenga amani ya kudumu.

Aidha, amezitaka nchi za ukanda huo kuwekeza katika kuwawezesha wanawake kiuchumi kwa kuwapatia fursa za elimu, mafunzo, mitaji, mikopo na masoko ili waweze kukuza biashara zao na kushiriki kikamilifu katika maendeleo.

Amesema kuwekeza kwa wanawake na vijana ni kuwekeza katika mustakabali wa amani na maendeleo ya ukanda wa Maziwa Makuu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.