Skip to main content

UWAMAKI WASITISHA HUDUMA ZA USAFIRISHAJI ZIWA TANGANYIKA

Na Tryphone Odace – Kigoma.

UWAMAKI WASITISHA HUDUMA ZA USAFIRISHAJI ZIWA TANGANYIKA

Na Tryphone Odace – Kigoma.

Umoja wa Wamiliki na Wasafirishaji wa Maboti Mkoani Kigoma (UWAMAKI), wanaofanya shughuli zao katika Ziwa Tanganyika, umesitisha kwa muda huduma za usafirishaji, ukilalamikia sheria na taratibu zinazowazuia kusafirisha abiria na mizigo kwa pamoja.

Hatua hiyo imekuja huku wamiliki na baadhi ya wafanyakazi wa vyombo hivyo wakieleza kuwa zuio hilo limewaweka katika mazingira magumu kiuchumi, ikiwemo kupoteza wateja na kupungua kwa kipato.

Akizungumza hii leo Septemba 3,2026 kuhusu hatua hiyo, Mwenyekiti wa UWAMAKI, Kashinye Adam, alisema umoja huo umefikia siku ya tatu tangu kusitisha huduma za usafirishaji na kwamba utaendelea na msimamo huo hadi mamlaka husika zitakapopatikana na kutoa ufumbuzi wa changamoto hiyo.

“Wamiliki wa vyombo hivyo wanahitaji suluhisho litakalowawezesha kuendelea na shughuli zao bila kuathiri maslahi ya wasafiri pamoja na usalama wa usafirishaji katika Ziwa Tanganyika na tunaendelea na mgomo hadi pale maamlaka zitakapotoa ufafanuzi” alisema Adam.

Naye Afisa Mfawidhi wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), Adam Mamilo, alisema changamoto hiyo imetokana na kuwepo kwa tofauti za sheria na taratibu za usafirishaji kati ya Tanzania na nchi jirani zinazozunguka Ziwa Tanganyika.

Alisema tofauti hizo zimekuwa zikisababisha changamoto katika utekelezaji wa taratibu za usafirishaji, hivyo kuna umuhimu wa mamlaka husika kushirikiana kutafuta suluhisho la kudumu.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Ujiji, Dkt. Rashid Chua Chua, aliwashauri wamiliki wa vyombo hivyo kuchagua aina moja ya huduma wanayotaka kutoa, kati ya kusafirisha abiria au kubeba mizigo, ili kuendana na matakwa ya sheria na taratibu zilizopo.

Hatua ya UWAMAKI kusitisha huduma imeibua mjadala kuhusu changamoto zinazowakabili watoa huduma za usafirishaji katika Ziwa Tanganyika, huku wananchi wanaotegemea usafiri huo wakitajwa pia kuathirika na kusimama kwa huduma hizo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.