Skip to main content

UWAJIBIKAJI: SOKO APEWA KONGOLE KWA KUSIMAMIA ILANI YA CCM

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

UWAJIBIKAJI: SOKO APEWA KONGOLE KWA KUSIMAMIA ILANI YA CCM

Na William Bundala, Kahama - Shinyanga.

Serikali Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, imempongeza Diwani wa Kata ya Majengo, Zacharia Soko kwa kutimiza wajibu wake  na kusimamia vyema ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM), kwa kuwahudumia wananchi kwa kutoa misaada mbalimbali katika shule za kata hiyo na kusimamia maendeleo.

Pongezi hizo, zimetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Frank Nkinda katika kikao cha wazazi wa wanafunzi wa kata ya majengo kilicholenga kuhamasisha uchangiaji wa chakula Shuleni.

Amesema, Soko amekuwa mstari mbele  kusimamia maendeleo katika kata yake kwa kuwa karibu na wananchi na kutekeleza vyema ilani ya chama cha Mapinduzi na kwamba anajitoa  sana katika kutoa misaada katika shule za kata.

“Nikupongeze sana Mh Diwani kwa kazi nzuri,umekuwa mstari wa mbele kusimamia maendeleo katika kata hii,mchango wako unaoutoa katika shule unasaidia sana kuongeza ufaulu,lakini pia umekuwa mstari wa mbele kunifikia mara kwa mara kunieleza kuhusu mahitaji ya maendeleo katika kata,” amesema Nkinda.

Katika hatua nyingine Nkinda ametoa wito kwa wazazi wa Kata ya Majengo kuchangia huduma ya chakula shuleni kwani watoto wengi wanasoma bila kupata chakula hali inayoweza kuwasababishia kufanya  vibaya kwenye mitihani yao.

“Nitoe wito kwa wazazi wenzangu tuchangie chakula kwa ajili ya watoto wetu,mtoto anapokaa bila kula kwa muda mrefu hawezi kuelewa masomo anayofundishwa,na suala la kula ni haki ya mwanafuzi maana ni shea yake ambayo hata angekuwa nyumbani angekula,” amesisitiza Nkinda.

Nao baadhi ya wazazi wenye wanafunzi katika shule ya sekondari Mama Samia wameiomba serikali kuongeza walimu katika Shule hiyo Pamoja na kuongeza walimu wa kiume kwani shule hiyo ina walimu wakiume wawili tu.

“Tunaiomba serikali ituongezee walimu katika shule yetu ya Mama Samia,shule ina walimu wachache na mbaya zaidi walimu wa kiume ni wawili tu jambo ambalo wanafunzi hawawheshimu walimu wa kike kwasababu hakuna sauti za kiume za kuwadhibiti,” Wamesema wananchi hao.

Katika kikao hicho Diwani Soko ametoa Mahindi gunia 15 kwa kila shule, Sukari kilo 75 na jezi za michezo, huku Mkuu wa wilaya ya Kahama Frank Nkinda akichangia kilo 500 za Mahindi katika shule hizo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.