Skip to main content

UVINZA YAPATA HATI SAFI UKAGUZI HESABU ZA SERIKALI 2024/2025

Na Faustine Kasala - Kigoma.

UVINZA YAPATA HATI SAFI UKAGUZI HESABU ZA SERIKALI 2024/2025

Na Faustine Kasala - Kigoma.

Mkuu wa Mkoa wa Kigoma IGP Mstaafu Balozi Simon Sirro,ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza kwa kupata hati safi katika ukaguzi wa hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025 pamoja na kupunguza idadi ya hoja za ukaguzi wa CAG hatua inayoashiria kuimarika kwa usimamizi wa fedha za umma. 

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani Balozi Sirro amewataka madiwani kuendelea kusimamia kwa ukaribu utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kata zao ili kuhakikisha amani na utulivu vinaendelea kudumishwa.

"Niwaombe Waheshimiwa Madiwani ongezeni juhudi katika  usimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali katika maeneo yenu na watumishi wengine wote wa Halmashauri hii ya Uvinza wote kwa pamoja endeleeni kudumisha amani pia na utulivu, uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu ili wananchi wafaidike na utumishi wenu" Alisema Sirro.

Balozi Sirro amesisitiza pia umuhimu wa kuendeleza zoezi la uandikishaji wa makazi, kuongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato kupitia ulipaji wa kodi, kubuni vyanzo vipya vya mapato sambamba na kushirikiana kudhibiti wahamiaji haramu, pamoja na kuzuia migogoro ya ardhi ambayo inaweza kuhatarisha amani na kuchelewesha maendeleo kwa wananchi.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Uvinza, Dinah Mathamani amesema Halmashauri imeendelea kuchukua hatua za kurekebisha mapungufu yaliyobainishwa na ukaguzi wa CAG, na kwamba ufuatiliaji wa karibu utaendelea kufanyika ili kuhakikisha hoja zilizobaki zinapatiwa ufumbuzi kwa wakati na kuimarisha zaidi utendaji wa kazi wa Halmashauri

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.