Skip to main content

UVCCM KAGERA YAZINDUA OPARESHENI VIDAFUSA SEASON 2 KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

Na Clavery Christiaan, Ngara - Kagera

UVCCM KAGERA YAZINDUA OPARESHENI VIDAFUSA SEASON 2 KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

Na Clavery Christiaan, Ngara - Kagera

Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Kagera, Faris Buruhani, ameanza rasmi Operesheni ya Vijana Daka Fursa na Samia (VIDAFUSA) Season 02 katika Kata ya Ngara Mjini, Wilaya ya Ngara, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuwawezesha vijana kutambua na kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana kupitia Serikali na taasisi za kifedha.

Akizungumza katika uzinduzi wa operesheni hiyo, Buruhani alisema lengo kuu la VIDAFUSA Season 02 ni kuwajengea vijana uwezo wa kutambua fursa zilizopo, kupata elimu ya fedha na uwekezaji pamoja na kuwaunganisha na taasisi zinazotoa huduma za mikopo na mitaji kwa ajili ya kuanzisha au kukuza shughuli za kiuchumi.

Alisema katika makongamano hayo, vijana wanapata elimu kutoka kwa maafisa wa wa taasisi z kifedha pamoja na Maafisa Maendeleo ya Jamii, ambao wanatoa ufafanuzi kuhusu taratibu za kupata mikopo, mbinu za uwekezaji na namna bora ya kutumia fursa mbalimbali za kiuchumi zinazotolewa na Serikali.

“VIDAFUSA ni jukwaa la vijana wote. Hatuangalii tofauti za itikadi za kisiasa, bali tunalenga kuwaunganisha vijana ili waweze kupata elimu na kunufaika na fursa zilizopo kwa ajili ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla,” amesema Buruhani.

Aidha, aliwahimiza vijana wa Mkoa wa Kagera kujitokeza kwa wingi kushiriki makongamano hayo ili kupata maarifa yatakayowasaidia kujiajiri, kuanzisha biashara na kuongeza kipato chao kupitia fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na taasisi za kifedha.

Kwa mujibu wa Buruhani, operesheni hiyo ni sehemu ya mkakati wa UVCCM Mkoa wa Kagera wa kuhakikisha vijana wanakuwa na uelewa wa kutosha kuhusu fursa za maendeleo na kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali ili kuchangia ukuaji wa uchumi wa mkoa na taifa kwa ujumla.

Operesheni hiyo itafanyika kwa siku 16 mfululizo katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera kupitia makongamano maalum ya fursa yatakayowakutanisha vijana na wadau mbalimbali wa maendeleo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.