Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Ummy Ally Mwalimu kuwa Mshauri wa Rais anayeshughulikia Masuala ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto.
Taarifa iliyotolewa hii leo Juni 2, 2026 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka imeeleza kuwa uteuzi huo umefanywa na Rais kwa lengo la kuimarisha usimamizi na utekelezaji wa masuala ya afya ya uzazi pamoja na ustawi wa mama na mtoto nchini.


Discussion
Reader comments
0 contributions