Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemteua Mansura Mosi Kassim kuwa Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Kabla ya Uteuzi, Mansura alikuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar, huku uteuzi huo ukianza hii leo Juni 22, 2026 na anatarajia kuapishwa rasmi Juni 24, 2025 saa 4:00 asubuhi Ikulu.

Discussion
Reader comments
0 contributions