Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya teuzi mbalimbali na kumteua Dkt. Juma Zuberi Homera kuwa Waziri wa Nishati, huku Masanja Kungu Kadogosa akiteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi.
Uteuzi huo umetangazwa kupitia taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, ambapo kabla ya uteuzi huo Dkt. Homera alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
Aidha, taarifa hiyo pia imeeleza kuwa, Dkt. Samia pia amemteua Abdallah Hamis Ulega, kuwa Waziri wa Katiba na Sheria, nafasi ambayo ilikuwa ikishikiliwa na Homera.


Discussion
Reader comments
0 contributions