Skip to main content

UTEUZI: HAJI MANARA MSEMAJI WA TIMU ZA TAIFA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amemteua Haji Manara kuwa msemaji wa timu zote za Taifa za mpira wa miguu nchini.

UTEUZI: HAJI MANARA MSEMAJI WA TIMU ZA TAIFA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amemteua Haji Manara kuwa msemaji wa timu zote za Taifa za mpira wa miguu nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo Mei 28, 2026, Waziri Makonda amesema uteuzi huo unalenga kuimarisha mawasiliano, hamasa pamoja na taswira ya timu za Taifa kwa wananchi na wadau wa michezo nchini.

Makonda amesema Haji Manara atafanya kazi chini ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ambapo atasimamia mawasiliano na kuzisemea timu zote za Taifa za mpira wa miguu.

Haji Manara.

Uteuzi huo unatajwa kuleta sura mpya katika eneo la mawasiliano ya michezo nchini kutokana na uzoefu mkubwa alionao Haji Manara katika masuala ya uhamasishaji, mahusiano ya michezo pamoja na mawasiliano ya vilabu vya soka nchini.

Hatua hiyo imeanza kuzua mijadala mbalimbali miongoni mwa wadau wa michezo huku wengi wakisubiri kuona namna atakavyotekeleza jukumu hilo jipya katika timu za Taifa za Tanzania.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.