Skip to main content

UTAPELI WA AJIRA Q-NET: DC GONDWE AOKOA VIJANA 125 SINGIDA

Vijana 125 kutoka mikoa 11 nchini wameokolewa wilayani Singida baada ya kudanganywa kwa ahadi ya ajira ya Q-Net yenye mshahara wa Sh. 300,000 hadi 600,000.

UTAPELI WA AJIRA Q-NET: DC GONDWE AOKOA VIJANA 125 SINGIDA
Studio Narration JAMBO FM

UTAPELI WA AJIRA Q-NET: DC GONDWE AOKOA VIJANA 125 SINGIDA

0:00 --:--

Vijana 125 kutoka mikoa 11 nchini wameokolewa wilayani Singida baada ya kudanganywa kwa ahadi ya ajira ya Q-Net yenye mshahara wa Sh. 300,000 hadi 600,000.

Vijana hao walikutwa wamekusanywa katika nyumba tatu, baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe kufanya msako huo.

Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe akizungumza kwa msisitizo kuhusu utapeli wa ajira kwa vijana 125.

Kwa mujibu wa maelezo yao, kila kijana alitakiwa kulipa Sh. 50,000 kwa ajili ya makazi yenye watu 30 hadi 50 kwa nyumba moja, huku wakidaiwa kupatiwa mafunzo ya wiki mbili hadi tatu.

Baadhi ya Vijana waliokokewa Wilaya ya Singida kufuatia utapeli wa ajira unaofanywa na taasisi ya Q-Net

Gondwe amesema wazazi wengi walikuwa wakipigiwa simu na kutakiwa kutuma fedha, na amewataka vijana na wazazi kufanya uhakiki wa taarifa za ajira kabla ya kusafiri.

Aidha, Gondwe ameipiga marufuku taasisi hiyo ya Q-Net Wilayani Singida na kumuagiza Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) kuwasaka na kuwakamata viongozi wake, akisema ni mara ya tatu kwa tukio kama hilo kujitokeza licha ya hatua zinazochukuliwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.