Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kumjeruhi Mzee Mihayo Budaga(78), wakimtuhumu kwa imani za kishirikina, tukio ambalo limeibua masikitiko kwa wananchi wa Wilaya ya Magu.
Taarifa ya Jeshi la Polisi Mkoani humo imeeleza kuwa, watuhumiwa hao wanadaiwa kuvamia nyumba ya mzee huyo iliyopo wilayani Magu usiku wa Julai 11, 2026 kisha kumshambulia kwa kutumia kitu chenye ncha kali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP Wilbrod Mutafungwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Mzee Mihayo kwasasa amelazwa katika Hospitali ya Bugando kwa matibabu, huku uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo ukiendelea.
Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea ili kuweza kuwafikisha Watuhumiwa Mahakamani.
Discussion
Reader comments
0 contributions