Skip to main content

USHETU WAZINDUZI SEKONDARI YA TATU KIDATO CHA TANO, SITA

Na William Bundala, Kahama - Ushetu.

USHETU WAZINDUZI SEKONDARI YA TATU KIDATO CHA TANO, SITA

Na William Bundala, Kahama - Ushetu.

Mbunge wa Jimbo la Ushetu, Emmanuel Cherehani amezindua rasmi Shule ya Sekondari Sabasabini (Kidato cha tano na sita) iliyopo Kata ya Sabasabini, Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.

Akizungumza katika hafla hiyo, Cherehani amesema mafanikio hayo yanatokana na jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuboresha sekta ya elimu na kusogeza huduma muhimu karibu na wananchi.

“Jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais wetu Dr.Samia Suluhu Hassan zilimeleta neema katika sekta ya elimu,ni hii ni kutokana kwamba huduma za elimu zimesogezwa siyo kama zamani sasa hivi watoto wetu hawasafiri umbali mrefu kupata elimu,” amesema Cherehani.

Pia ameahidi kushirikiana na serikali kutatua changamoto ya maji kwa kuhakikisha kisima kinachimbwa shuleni hapo ilikuwaondolea adha wanafunzi ya kufuata maji umbali mrefu.

“Tazizo la ukosefu wa maji hapa shuleni ni kubwa,mama samia ameleta mtambo wa kuchimba visima katika mkoa wetu wa Shinyanga tutahakikisha tunachimba kisima katika shule hii,mabomba yote ya kusafirisha maji nitatoa mimi.” Ameongeza Cherehani.

Awali, akisima taarifa ya mradi huo Mkuu wa shule ya sekondari Sabasabini Yona Mtinda, amesema shule imepokea zaidi ya Shilingi milioni 617.4 zilizotumika kujenga madarasa, vyoo na bweni la wavulana, hatua iliyowezesha shule hiyo kupandishwa hadhi na kuanza kutoa elimu ya Kidato cha Tano na Sita.

“Tunaishukuru serikali kwa mchango mkubwa katika ujenzi wa shule hii,tulipokea kiasi cha shilingi milioni 617 ambazo tumejenga madarasa,vyoo na bweni la wavulana hali iliyopelekea shule yetu kupandishwa hadhi,” amesema Mtinda.

Naye Katibu wa CCM Wilaya ya Kahama, Andrew Chatwanga amesema, maendeleo yanayoonekana katika Jimbo la Ushetu ni matokeo ya utekelezaji wa Ilani ya CCM na viongozi wanaowajibika kwa wananchi.

“Niwapongeze sana viongozi wetu mkiongozwa na mbunge wenu mnafanya kazi nzuri katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi,ujenzi huu ni wazi kuwa viongozi wanajua wanachokifanya kwa wananchi hao,” smesema Chatwanga.

Halmashauri ya Ushetu kwa sasa ina shule tatu za kidato cha tano na cha sita ambayo ni Dakama Sekondari,Mweli sekondari Pamoja na Sabasabini Sekondari.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.