Skip to main content

USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU UNAWATESA WATOTO WA KIKE - BI. REHEMA

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

USAFIRISHAJI HARAMU WA BINADAMU UNAWATESA WATOTO WA KIKE - BI. REHEMA

Na Eunice Kanumba – Shinyanga.

Usafirishaji haramu wa binadamu (TIP), umetajwa kuwa ni moja ya changamoto  inayosumbua  wasichana kutoka maeneo ya vijijini kwenda mjini kwa ahadi za kupatiwa ajira,elimu au maisha bora  na baadaye wanaishia katika mazingira ya unyonywaji na unyanyaswaji  na wakati mwingine hupelekea hata kupoteza maisha.

Hayo yamesemwa na  Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga ambaye ni  Ofisa Maendeleo ya Jamii Rehema Edson  katika  semina ya mafunzo juu ya Usafirishaji  haramu wa binadamu  na uhamiaji salama  kwa maafisa wa  serikali  katika mradi wa EmPoWeRed II  unaotekelezwa na shirika la CVM and APA  Kwa ushirikiano wa Chodawu,Wote sawa   kwa kufadhiliwa na shirika la Kimataifa  la Italian Agency for Development Cooperation.

Rehema amesema   kwa bahati mbaya  watoto wengi hususani wasichana  balehe ambao walitakiwa kuwa shuleni huishia  kudanganywa kwa kusafirishwa kufanya  kazi za nyumbani katika nyumba binafsi ambapo hukumbana  na changamoto nyingi.

“Changamoto wanazokumbana nazo   mojawapo ni masaa mengi ya kufanya kazi bila mapumziko,malipo duni au kutolipwa kabisa,kunyimwa haki ya elimu,unyanyasaji wa kimwili na kisaikolojia na  unyonywaji wa kiuchumi,” amesema Rehema.

Ameongeza kuwa   changamoto hii ni kubwa zaidi kwa sababu kazi za majumbani  binafsi zinawafanya waathirika kuwa wagumu kutambulika kwa haraka  ikiwa pia wamekuwa wakishuhudia  aina nyingine ya ajira za watoto kufanya kazi mashambani, shughuli za ufugaji, uchimbaji mdogo wa madini, biashara  zisizo rasmi na uuzaji wa bidhaa mitaani.

“Wahalifu wa sasa wamebadilisha  mbinu  hawategemei tena madalali wa kawaida  pekee wanatumia  tecknolojia,mitandano ya kijamii, matangazo ya ajira ya uongo na mifumo isiyo rasmi ya uajiri,” ameongeza Rehema.

Naye mwezeshaji kutoka. shirika la CVM Mwajuma  Ally amesema Mradi huu  umeanza  awamu ya pili  baada ya kuonekana mafanikio makubwa na utatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu  kuanzia mwaka 2026  ambao umelenga hasa kwa  wasichana na kuangalia wasichana wa kazi za nyumbani kuweza kujiendeleza kupitia vyuo vya mafunzoi  na kupewa mikataba ya ajira na waajiri wao

Mwezeshaji wa Semina hiyo kutoka Wizara ya Mambo ya  Ndani, Providence  Simbila  amesema usafirishaji haramu wa binadamu ni kosa la kisheria kwa mujibu wa sheria zilizopo ndani ya nchi ya Tanzania  na anayefanya kazi ya usafirishaji huo anakuwa na viashiria vya mambo matatu ambavyo vinaweza kubainika.

"Mambo hayo  mojawapo ni matendo yanayotumika kumfanya akubali  kusafirishwa, Mbinu  za ahadi ya uongo kama mshahara mzuri na kazi nzuri  ya  muda mfupi ,Vitisho kwa lengo la  kwenda kumfanyia kazi na kumnufaisha,” amesema Simbila.

 Serikali na jamii zinaendelea kushirikiana kupambana na uhalifu huu kwa kutoa elimu, kuimarisha usalama na kuwachukulia hatua za kisheria wahusika. Wananchi wanahimizwa kuwa waangalifu na kutoa taarifa kwa mamlaka wanapobaini vitendo vinavyohusiana na usafirishaji haramu wa binadamu.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.