Skip to main content

USAFI NI MUHIMU KWA ULINZI WA AFYA ZA WANANCHI - MEYA MDAMA

Na Saulo Stephen - Singida.

USAFI NI MUHIMU KWA ULINZI WA AFYA ZA WANANCHI - MEYA MDAMA

Na Saulo Stephen - Singida.

Mstahiki Meya Wa Manispaa ya Singida, Godfrey Mdama amewaasa wananchi kutambua umuhimu na kuendeleza utamaduni wa kufanya usafi mara kwa mara, ili kulinda afya za wananchi na kudumisha hadhi ya Manispaa hiyo.

Meya Mdama ameyasema hayo Machi 28, 2026 wakati alipoongoza watumishi wa Manispaa ya Singida pamoja na wananchi wa Kata ya Misuna katika zoezi la kufanya usafi kwenye eneo la Stendi ya Mabasi Misuna Mjini Singida.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Godfrey Mdama akishiriki zoezi la usafi katika eneo la Stendi kuu ya Mabasi Misuna, mjini Singida.

Amebainisha kuwa hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha mazingira bora na kudhibiti changamoto za uchafu hususan katika maeneo yenye mikusanyiko mikubwa ya watu ikiwemo eneo hiloa la Stendi kuu ya mabasi.

Aidha zoezi hilo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na wananchi wa Kata ya Misuna kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi hilo, na hivyo kuonyesha mwamko na ushirikiano katika utunzaji wa mazingira.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, JoanFeith Kataraia akishiriki zoezi la usafi katika eneo la Stendi kuu ya mabasi Misuna, Singida.

Katika zoezi hilo, Meya Mdama aliambatana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida, Bi. Joanfaith Kataraia, Naibu Meya, madiwani, pamoja na Wakuu wa Divisheni na Vitengo kutoka Manispaa hiyo.

Wananchi wa Misuna Manispaa ya Singida wakiwa katika zoezi la usafi, Stendi kuu ya mabasi Misuna, Singida.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.