Skip to main content

UPOTEVU WA NYETI: POLISI WAKEMEA UZUSHI, IMANI ZA KISHIRIKINA

Jeshi la Polisi Nchini, limekemea vitendo vya hivi karibuni vilivyojitokeza, kwa tabia za baadhi ya watu na mashabiki wao kuwatuhumu watu wengine kuwa, wamewashika mabegani watu fulani na sehemu zao za siri kutoweka.

UPOTEVU WA NYETI: POLISI WAKEMEA UZUSHI, IMANI ZA KISHIRIKINA

Jeshi la Polisi Nchini, limekemea vitendo vya hivi karibuni vilivyojitokeza, kwa tabia za baadhi ya watu na mashabiki wao kuwatuhumu watu wengine kuwa, wamewashika mabegani watu fulani na sehemu zao za siri kutoweka.

Taarifa ya Msemaji wa Jeshi hilo Nchini, David Misime imeeleza kuwa, tabia hizo zinazoongozwa na imani za kishirikina zilianza kuibuka maeneo ya Tunduma Mkoa wa Songwe Aprili 1, 2026 na kusababisha vifo vya watu watano na wengine wawili kujeruhiwa.

DCP. David Misime.

"Tabia hiyo pia imejitokeza Aprili 3,2026 huko Makongolosi na Mtaa wa Maendeleo Jijini Mbeya ambapo watu wawili walishambuliwa na kujeruhiwa na hivi sasa wanaendelea na matibabu hospitalini," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha, ameeleza kuwa matukio kama hayo pia yametokea eneo la Kimara Mwisho na Mbezi Shule Jijini Dar es Salaam Aprili 3, 2024 majira ya jioni ambapo watu wawili wanaume
nao walituhumiwa kuwa, wamewagusa watu mabegani na matokeo yake sehemu zao za siri zikatoweka.

"Leo Aprili 4,2026 katika Jiji la Mbeya kumejitokeza tena matukio mengine mawili
yaliyotokea eneo la Kabwe Wilaya ya Mbeya Mjini na Double J Kalumbulu Wilaya ya Kyela ambapo watu wawili wamajeruhiwa kwa tuhuma hizo hizo za uzushi ambapo mmoja wa anayedai kufanyiwa hivyo alipofanyiwa uchunguzi na
Madaktari sehemu zake zilikutwa zipo na hazina tatizo lolote," ilielezwa.

Misime kupitia taarifa hiyo ameeleza kuwa, "tabia hizi zinazoongozwa na imani za kishirikina, mihemko ya kishabiki na
malengo ambayo hayaja bainika hazina ukweli wowote kwani wanaodaiwa kuguswa bega na sehemu zao za siri kutoweka walipokaguliwa sehemu zao za siri zilikutwa zikiwa maeneo yake kama kawaida na maeneo mengine.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.