Skip to main content

UPINZANI WATAKA MIUNDOMBINU MJI WA SERIKALI DODOMA IIMARISHE UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI

Viongozi wa vyama vya upinzani nchini wameridhishwa na miundombinu ya kisasa iliyojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, huku wakisisitiza kuwa miundombinu hiyo inapaswa kwenda sambamba na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

UPINZANI WATAKA MIUNDOMBINU MJI WA SERIKALI  DODOMA IIMARISHE UTOAJI HUDUMA KWA WANANCHI
Studio Narration JAMBO FM

UPINZANI WATAKA MIUNDOMBINU MJI WA SERIKALI DODOMA IIMARISH...

0:00 --:--

Viongozi wa vyama vya upinzani nchini wameridhishwa na miundombinu ya kisasa iliyojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, huku wakisisitiza kuwa miundombinu hiyo inapaswa kwenda sambamba na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Viongozi hao wamesema kukamilika kwa majengo ya wizara na taasisi mbalimbali za Serikali ni matunda ya kodi za Watanzania, hivyo ni muhimu miundombinu hiyo kutunzwa na kutumiwa ipasavyo ili kuleta manufaa yaliyokusudiwa kwa wananchi.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 29, 2026, na Katibu Mkuu wa Chama cha UDP, Saum Rashid, alipotembelea majengo ya wizara, taasisi za Serikali na miundombinu ya barabara katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, akiwa ameambatana na viongozi wa vyama vingine vya upinzani nchini.

Ziara hiyo imefanyika siku moja kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuzindua majengo na miundombinu ya Mji wa Serikali Mtumba.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Saum amewataka Watanzania kushirikiana katika kutunza miundombinu hiyo iliyojengwa kwa fedha za ndani, huku akihimiza umoja na utulivu nchini.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha AAFP, Rashid Rai, ameishukuru Serikali kwa kukamilisha ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba, akisisitiza kuwa watumishi wote wa Serikali wanapaswa kuhamia katika eneo hilo ili majengo na miundombinu iliyowekezwa itumike ipasavyo na kuleta matokeo yaliyokusudiwa.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.