Skip to main content

UPIMAJI WA AFYA YA UDONGO KUONGEZA TIJA YA KILIMO KATAVI

Na Daniel Gahu - Katavi.

UPIMAJI WA AFYA YA UDONGO KUONGEZA TIJA YA KILIMO KATAVI

Na Daniel Gahu - Katavi.

Ikiwa msimu wa kilimo ukielekea ukingoni, wakulima mkoani Katavi wanatarajiwa kunufaika na matumizi sahihi ya mbolea na kuongezeka kwa tija ya uzalishaji kupitia zoezi la upimaji wa afya ya udongo linaloendeshwa na Wizara ya Kilimo katika halmashauri zote za mkoa huo.

Akizungumza katika kikao cha tathmini ya zoezi hilo kilichofanyika mkoani Katavi, Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Matumizi ya Ardhi ya Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Florian Kalemela, amesema sampuli za udongo zinazokusanywa zitapelekwa maabara kwa ajili ya uchakataji na upembuzi ili kubaini virutubisho vilivyopo na vinavyokosekana katika udongo.

“Matokeo ya uchambuzi wa sampuli hizi yatasaidia kubaini afya ya udongo katika maeneo mbalimbali na kutoa mwongozo wa matumizi sahihi ya mbolea kulingana na mahitaji ya kila eneo,” amesema Kalemela.

Kwa upande wake, Dkt. Sibaway Mwango, mtaalamu bobezi wa udongo kutoka TARI, amesema zoezi hilo linaendelea vizuri ambapo timu mbili zimekuwa zikikusanya sampuli za udongo katika kina cha futi mbili na mita mbili kwa lengo la kutathmini rutuba ya udongo, kubaini aina mbalimbali za udongo uliopo na kutoa mapendekezo ya mbolea zinazofaa kutumika katika maeneo husika.

Akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi hilo, Afisa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Consolatha Chambi, amesema zoezi lilianza Juni 16, 2026 na linahusisha halmashauri zote za Mkoa wa Katavi ambapo taarifa zitakazopatikana zitasaidia kubaini mazao yanayofaa kulimwa katika maeneo husika badala ya wakulima kuendelea kulima kwa mazoea.

“Tunatarajia kuwabadilisha wakulima wa Katavi kutoka kilimo cha mazoea kwenda kilimo chenye tija, kitakachopunguza gharama za uzalishaji, kuongeza mavuno na kuinua kipato cha wakulima,” amesema Chambi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.