Skip to main content

UMEME WA REA WACHOCHEA MAENDELEO HOLILI, WACHIMBAJI WAOMBA HUDUMA IFIKE MAENEO YOTE YA MACHIMBO

Wakazi na wachimbaji wa matofali ya mawe katika eneo la Holili, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, wameendelea kuishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuwafikishia huduma ya umeme, huku wakiomba huduma hiyo kuendelea kusambazwa katika maeneo yote ya machimbo, ili kunufaisha wachimbaji wengi zaidi.

UMEME WA REA WACHOCHEA MAENDELEO HOLILI, WACHIMBAJI WAOMBA HUDUMA IFIKE MAENEO YOTE YA MACHIMBO

Wakazi na wachimbaji wa matofali ya mawe katika eneo la Holili, wilayani Rombo mkoani Kilimanjaro, wameendelea kuishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuwafikishia huduma ya umeme, huku wakiomba huduma hiyo kuendelea kusambazwa katika maeneo yote ya machimbo, ili kunufaisha wachimbaji wengi zaidi.

Wamesema umeme umekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo kwa kuongeza ufanisi wa uzalishaji na kuboresha maisha ya wananchi wanaojishughulisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Akizungumza katika eneo la machimbo, mchimbaji wa matofali ya mawe Peter Kimuya maarufu kama Mzee Zungu amesema kuwa ujio wa umeme wa REA umeleta mapinduzi makubwa katika shughuli za uchimbaji na uchakataji wa matofali kwa kuwa sasa wanaweza kutumia mitambo ya kisasa inayoongeza kasi na ubora wa uzalishaji.

“Kabla ya umeme kufika tulikuwa tunatumia njia za kawaida ambazo zilikuwa zinachukua muda mwingi na gharama kubwa, lakini sasa tuna uwezo wa kuzalisha matofali mengi kwa muda mfupi na kwa ufanisi mkubwa,” amesema Mzee Zungu.

Naye Robert Riziki, mmoja wa vijana wanaofanya kazi katika machimbo hayo, amesema kuwa maeneo yaliyopata umeme tayari yameonyesha matokeo chanya kwa kuongeza uzalishaji na fursa za ajira kwa vijana.

“Kwa kweli umeme wa REA umetusaidia sana. Kupitia kazi hii nimeweza kupata kipato kizuri, kujenga nyumba yangu na kufungua duka la jezi ambalo linaniingizia kipato cha ziada na kunisaidia kuendesha maisha yangu ya kila siku,” amesema Robert Riziki.

Aidha, Mzee Zungu amewahamasisha vijana kuchangamkia mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali kupitia halmashauri ili waweze kuanzisha au kupanua shughuli zao za uzalishaji na kujiongezea kipato.

Kwa upande mwingine, baadhi ya wachimbaji akiwemo Gasper Mroso, Timothy Mangi na Honorath Maswei wameeleza kuwa bado kuna maeneo ya machimbo yanayokabiliwa na changamoto ya kukosa umeme, jambo linalowalazimu kutumia zana duni na mbinu za kawaida katika kazi zao.

Wamesema hali hiyo husababisha uzalishaji kuwa mdogo, kuongeza gharama za uendeshaji pamoja na kuweka maisha yao katika hatari ya kupata majeraha wanapotekeleza shughuli za uchimbaji.

Wachimbaji hao wameiomba REA kuendelea kupanua miundombinu ya umeme katika maeneo yaliyobaki ili kuwawezesha kutumia vifaa vya kisasa vya uchimbaji na uchakataji wa matofali.

Wamefafanua kuwa upatikanaji wa umeme utarahisisha kazi, kupunguza muda wa uzalishaji, kuongeza tija na kuboresha kipato cha wachimbaji pamoja na kuchochea maendeleo ya kiuchumi katika eneo la Holili.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.