Skip to main content

ULEMAVU, HALI YA KIFEDHA USIMKOSESHE MTU MATIBABU - WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amtaka pasitokee mtu kukosa matibabu kwa sababu ya ulemavu au hali yake ya kifedha.

ULEMAVU, HALI YA KIFEDHA USIMKOSESHE MTU  MATIBABU - WAZIRI MKUU

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amtaka pasitokee mtu kukosa matibabu kwa sababu ya ulemavu au hali yake ya kifedha.

Mwigulu ameyasema hayo hii leo Novemba 5, 2026 Bungeni jijini Dodoma na kuongeza kuwa Taasisi zetu ziendelee kutumia dirisha la msamaha kuwahudumia wenye mahitaji maalumu.

Amesema, "wenye mahitaji maalumu ambao bado hawajaingia katika mfumo wa bima ya afya, waendelee kutumia dirisha la msamaha huku tukiendelea na uandikishaji na kuwahamasisha Watanzania wote kujisajili."

Aliyamesema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Stella Alex Ikupa, kuhusu upatikanaji wa matibabu kwa watu wenye ulemavu ambao bado hawajafikiwa na mpango wa bima ya afya kwa wote.

Ilikuwa ni wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, katika Mkutano wa Tano, Kikao cha Nane cha Bunge la 13.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.