Skip to main content

UJENZI KITUO CHA AFYA SANGAMWALUGESHA KUWANUFAISHA WAKAZI 7,000 MASWA

Na Saada Almasi, Maswa - Simiyu.

UJENZI KITUO CHA AFYA SANGAMWALUGESHA KUWANUFAISHA WAKAZI 7,000 MASWA

Na Saada Almasi, Maswa - Simiyu.

Wakazi 7,000 waishio katika kata ya Sangamwalugesha Wilayani Maswa mkoani Simiyu wanakwenda kuondokana na kadhia ya kutokuwa na kituo cha afya baada ya serikali kutoa kiasi cha shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa zahanati .

Kukosekana kwa kituo cha afya katika eneo hilo, kumewaathiri zaidi wanawake wajawazito ambao haikuwa mara moja tu kupoteza watoto wao hasa pale ambapo walishindwa kutembea umbali wa kilometa 30 hadi 40 kufuata huduma Lalago ama Meatu na endapo ikitokea wamejifungua njiani na kukosa huduma za haraka hupelekea kupoteza watoto wao.

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Mwang’onda akiwa wilayani humo akitokea wilaya ya Meatu amezindua Kituo cha Afya Sangamwalugesha, kilichojengwa kwa shilingi milioni 250 kilichotarajiwa kuokoa maisha ya wakazi hao ambapo kiongozi huyo baada ya kuridhishwa na ujenzi huo ameelekeza kianze kufanya kazi ndani ya wiki mbili.

“Niwapongeze sana kwa kusimamia ipasavyo ujenzi wa kituo hiki cha afya  lazima mtambue kwamba serikali yetu inajali sana wananchi wake na ndiyo maana inaelekeza fedha hizi kuja kuhudumia wananchi,kwa hatua iliyofikiwa sasa sioni tatizo la kutoanza kufanya kazi nielekeze vifaa tiba vipatikane viletwe ili wananchi waanze kupata huduma kuanzia siku 14 zijazo ili adha walizozipitia zifike ukomo, ” amesema Mwang’onda.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Maisha Mtipa amesema kuwa jengo la zahanati hiyo limekamilika ndani ya miezi sita na hivi sasa mpango uliopo ni kusubiri bajeti ya mwaka 2026/2027 ili waweze kuweka vifaa tiba haraka iwezekanavyo na wananchi waanze kupata huduma.

“Tumeanza kujenga jingo la wagonjwa wan je, vyoo na kichomea taka na kwa bajeti ya mwaka huu tutapata pesa kwa ajili ya vifaa tiba tuweke na baadae tutaleta watumishi, ili huduma zianze kutolewa haraka iwezekanavyo kwa wananchi,hivyo niishukuru serikali yetu kwa kuliona hili na kutupatia fedha ili wananchi wasiendelee kukosa huduma za afya,” amesema Mtipa.

Katika mahojiano ya awali ya Jambo FM na baadhi ya wananchi wa kata hiyo wananchi hao wametoa ya moyoni wakiishukuru serikali kwa kuwatizama kwa jicho la tatu wakisema kuwa waliyokuwa wakipitia yalikuwa magumu kuvumilika.

“Haijawa mara ya kwanza kupoteza watoto wetu kwa kujifungulia njiani tumekuwa tukipata huduma kituo cha afya Lalago ama tuende Meatu na usafiri tunaoutumia ni bodaboda ama ukiwa na uwezo ukodi gari likupeleke hospitali kubwa Meatu ,sasa unaweza ukajifungulia njiani halafu mtoto anaishia kupoteza maisha maana msaada wa haraka unakosa,kwa kujengewa kituo hiki tunaishukuru sana serikali,” amesema Rahel Mkwere mkazi wa Sangamwalugesha.

Kwa upande wake Veronica Mayenga amesema, “tulikuwa tunateseka sana hiki kituo kinakuja kutuokoa sana sisi akina mama pamoja na watoto wetu kwa sababu mimi mwenyewe wakati wa kujifungua mtoto wangu huyu nilitembea karibu masaa mawili kufuata huduma kituo cha afya Lalago."

Ukiwa wilayani humo  Mwenge wa Uhuru umekimbizwa umbali wa kilometa 138 na kuzindua miradi mitatu ,mawe ya msingi miradi miwili pamoja na kutembelea miradi miwili yenye thamani ya shilingi Bilioni 2.6.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.