Skip to main content

UJENZI SHULE YA SEKONDARI KALAGO YA BUSEGA KUTUMIA TSHs MILIONI 500

Na Saada Almasi, Busega - Simiyu.

UJENZI SHULE YA SEKONDARI KALAGO YA BUSEGA KUTUMIA TSHs MILIONI 500

Na Saada Almasi, Busega - Simiyu.

Wakazi wa kijiji cha Kalago wilayani Busega mkoani Simiyu, wanatarajia kupata unafuu wa watoto wao kupata elimu ya sekondari karibu na makazi yao kufuatia kiasi cha shilingi milioni 500 kutoka serikalini kilichotolewa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari.

Awali, Wanafunzi wa kijiji hicho na vijiji jirani walitegemea kusoma katika shule ya sekondari Lamadi na Anthony Mtaka ambazo ili kuzifikia iliwalazimu wazazi kuwapatia nauli za kuwafikisha watoto shuleni hapo na wakati mwingine kutembea umbali mrefu kwa wale ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwapatia pesa kwa ajili ya usafiri.

Jambo FM imezungumza na baadhi ya wazazi ambao wamekiri kutokuwepo kwa shule hiyo kijijini kwao kwa kiasi fulani kunachangia ufaulu mdogo kwa wanafunzi na wengine kukosa kufika shule hasa vipindi vya mvua.

“Hawa watoto wanajitahidi kufika shule hata kama kuna umbali lakini ni mateso kwao wazazi walio na uwezo watawapa watoto wao nauli lakini wengine hawana mtoto analazimika kutembea bila kujali umbali maana anapokosa shule siku nyingi anakuta wengine wako mbele,” amesema Zungu Kaswahili mkazi wa Kalago.

Naye mkazi wa Kata ya Lamadi, Christina Kabaka amesema, “ikifika kipindi cha mvua hadi watoto unawahurumia kwa maana wanakuwa wanafika nyumbani wakiwa wamelowa hadi daftari zao bora hata ingekuwa ni karibu wangesubiri mvua ikakata wakarudi lakini wakiona muda si rafiki na wanakoenda ni mbali wanalazimika kuja hivyohivyo wananyeshwa, tunashukuru serikali kuliona hili na kutuletea fedha za ujenzi.”

Akiwasilisha taarifa za fedha kwa wakazi wa kata hiyo, Diwani wa Kata ya Lamadi, Joseph Goryo amesema, hatua ya Serikali kutoa fedha hizo inalenga kuwaondolea wananchi adha wanazopitia Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Lamadi na Anthony Mtaka, ikiwemo mlundikano wa unaotokana na ufinyu wa Madarasa.

“Mradi huu utaanza hivi punde na kwa kushirikiana nanyi wananchi ni imani yangu mtatoa ushirikiano mzuri pale ambapo mtahitajika kwa manufaa ya watoto wetu ili tukamilishe mradi huu kwa wakati,” amesema Joseph Goryo.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.