Skip to main content

UJENZI MIRADI YA MAENDELEO BUKOBA IKAMILIKE KWA WAKATI - DKT. KIJAJI

Na Cecilia Shiratu, Bukoba - Kagera.

UJENZI MIRADI YA MAENDELEO BUKOBA IKAMILIKE KWA WAKATI - DKT. KIJAJI

Na Cecilia Shiratu, Bukoba - Kagera.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, amewataka Wakandarasi wanaotekeleza Miradi mbalimbali ya maendeleo katika Manispaa ya Bukoba, kuhakikisha wanaikamilisha kwa wakati, ili wananchi waanze kunufaika na huduma zinazotarajiwa kutolewa.

Dkt. Kijaji, ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi mbalimbali inayojengwa katika Manispaa ya Bukoba, ikiwemo soko kuu la kisasa, stendi kuu ya mabasi, barabara za kiwango cha lami zenye urefu wa kilometa 10, jengo la Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba na vyumba vya madarasa na mabweni katika Shule ya Sekondari Tunamkumbuka.

Amesema, Serikali imewekeza fedha nyingi katika miradi hiyo, hivyo ni wajibu wa Wakandarasi kuhakikisha inakamilika kwa ubora na ndani ya muda uliopangwa, ili iweze kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kuboresha huduma kwa Wananchi.

Akitoa taarifa kuhusu ujenzi wa soko kuu la kisasa, Mhandisi Mnyala Mwambungu alisema mradi huo ulianza Agosti 2025 na unatarajiwa kukamilika Januari 2027, ukiwa na muda wa utekelezaji wa miezi 15.

Alisema hadi sasa ujenzi umefikia asilimia 50, huku mkandarasi akiwa amelipwa asilimia 22.2 ya thamani ya mkataba.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mwambungu, kuchelewa kwa baadhi ya hatua za ujenzi kumesababishwa na changamoto za mvua kubwa pamoja na kazi ya usawazishaji wa eneo la mradi katika hatua za awali.

Aliongeza kuwa, soko hilo litakapokamilika litakuwa na zaidi ya maduka 224 na kuongeza uwezo wa kuhudumia wafanyabiashara kutoka takribani 2,000 wa sasa hadi zaidi ya wafanyabiashara 2,400, hatua inayotarajiwa kuboresha mazingira ya biashara na kuongeza mapato ya Halmashauri pamoja na Wananchi.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.