Skip to main content

UJENZI DARAJA LA MWAMANONGU KUONGEZA FURSA ZA KIUCHUMI MEATU, BILIONI 6 KUTUMIKA

Na Saada Almasi, Meatu - Simiyu.

UJENZI DARAJA LA MWAMANONGU KUONGEZA FURSA ZA KIUCHUMI MEATU, BILIONI 6 KUTUMIKA

Na Saada Almasi, Meatu - Simiyu.

Serikali imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la mto Mwamanongu lililopo kata ya Mwamanongu Wilayani Meatu mkoani Simiyu, ambalo ni uti wa mgongo kwa vijiji zaidi ya sita ambavyo vinalitegemea kwa shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii .

Utengenezaji huo unafuati adha ya muda mrefu wa wakazi wa vijiji hivyo kupitia baada ya daraja lililokuwepo kukatika na kukata mawasiliano kati ya pande mbili zinazotegemeana huku likiacha wakazi hao kugharamika zaidi pale ambapo wanahitaji huduma za kijamii ama kupeleka biashara baada ya gharama za usafiri kupanda.

Katika mkutano wa pamoja uliowahusisha viongozi wa serikali na wananchi wa kata hiyo, baadhi yao wameeleza adha kubwa wanazopitia hasa pale ambapo ni kipindi cha masika na wanahitaji huduma upande wa pili.

“Lile daraja tulikuwa tunalitegemea sana kutoa bidhaa zetu kutoka Mwanhuzi kuwa Mwamagembe  na hata huduma za afya pia lakini kwa sasa mtaji wangu umedorora ukianza kusafiri lazima uzunguke upande mwingine ambapo ni mbali ama uchukue pikipiki kwa gharama kubwa,” alibainisha Malile Kashinje.

“Hata wasafiri wamepungua sana kwenda sehemu zingine maana nauli zilikuwa ni ndogo ila baada ya mvua kuharibu hili daraja gharama zimekuwa juu sana ,sasa ikiendelea hivi hali itazidi kuwa ngumu kwa upande wetu,” amesema Malole.

“Hapa kwetu kuna zahanati tu hakuna kituo cha afya ikitokea mtu anaumwa uchungu au shida kubwa ambao itakuhutaji labda uongezwe damu huwezi kupata maana daraja limekatika kuvuka mto ni shida ,tunaiomba serikali itusaidie sisi wamama shida maana daraja litakapokuwa vizuri tunakuwa na unayoipitia ni kubwa,” amesema Asteria.

Akitolea ufafanuzi malalamiko hayo meneja wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) mkoani Meatu Elieza Mayengo amewahakikishia wananchi hao kuwa tayari serikali ipo katika m[pango wa kufanya ujenzi wa daraja kubwa na la kudumu ambao litakwenda kumaliza kabisa tatizo hilo.

“Napenda niseme kuwa tayari usanifu umefanyika na mapitio ya michoro yameanza kufanyika na baada ya hapo mkandarasi atatafutwa ili ujenzi uanze kufanyika na daraja linalokwenda kujengwa litakuwa na ubora mkubwa.”

Ameongeza”Hapo awali hatukuona hajakubwa ya kutengeneza daraja la chini wakati kuna mradi mkubwa unakuja kufanyika na hili litakalojengwa litakuwa kubwa na mfano wake ni lili la mto Itembe maana serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 6 ili wananchi mpate huduma hii,” amesema Mayengo.

Daraja la Mwamanoni, linategemewa na wananchi wa kijiji cha Mwamanoni ,Mwangikulu ,Mwabuzo ,Mwabalebi ,Mwambiti ,Mwamagembe pamoja na Mwamatiga kusafiri kutoka upande mmoja kwenda mwingine.

Join the conversation

What do you think about this story?

Share a useful perspective and keep the discussion respectful.

Keep reading

View all news
ON AIR
Jambo Assistant Tayari kukusaidia
JAMBO FM INTELLIGENCE

Kikomo cha maswali 6 kimefikiwa.Jaribu tena baada ya .
Utafiti utafunguka kwenye ukurasa kamili

Majibu ya AI yanaweza kuwa na makosa.