Katika kuboresha miundombinu ya barabara, ujenzi wa barabara ya Karakana–Mungumaji–Arusha yenye urefu wa kilomita 1.5 unaendelea ndani ya Manispaa ya Singida, ambapo kwa sasa mafundi wanaendelea na kazi ya kuweka tabaka la kokoto ngumu (Sub-base) kwa kutumia malighafi ya CRR.
Hatua hiyo ni sehemu muhimu ya maandalizi ya barabara hiyo kabla ya kuanza kwa kazi ya uwekaji wa lami, inayolenga kuifanya barabara hiyo kuwa katika kiwango kinachokusudiwa kupitia mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya miji wa TACTIC.
Baada ya kukamilika kwa uwekaji wa tabaka la Sub-base, hatua inayofuata itakuwa kunyunyizia lami ya awali (Prime Coat), kabla ya kufuatiwa na uwekaji wa lami ngumu aina ya Asphalt Concrete AC14.
Ujenzi wa barabara hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa TACTIC ndani ya Manispaa ya Singida, unaolenga kujenga jumla ya kilomita 7.579 za barabara kwa lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri na kurahisisha shughuli za kila siku za wananchi.
Discussion
Reader comments
0 contributions